SERIKALI YAJIVUNIA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA LUSHOTO
Picha ya pamoja ya meza kuu na wajumbe wa Menejimenti ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto pamoja na Watumishi wa chuo hicho.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Lusajo
Mwakabuku & Felix Chakila - WKS
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Chuo cha Uongozi wa
Mahakama Lushoto - IJA ni chuo cha mfano wa kuigwa katika utoaji wa mafunzo elekezi
ya awali na mafunzo endelevu ya kimahakama kwa kuzingatia Sera ya Mafunzo ya
Mahakama ya Mwaka 2019 ambayo inakitambua Chuo hicho kama kitovu au kisima cha
utoaji mafunzo kwa watumishi wa Mahakama.
Dkt.
Ndumbaro ameyasema hayo Tarehe 6 Machi, 2023 alipotembelea Chuo hicho na
kuzungumza na Uongozi wa Chuo, Menejimenti ya watumishi na Wafanyakazi wa IJA
na kuongeza kwamba Wizara ya Katiba na Sheria inajivunia kwa uwepo wa chuo
hicho ambacho kimebeba taswira ya nchi hususan kwa nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambapo kimeendelea kuwa mfano wa kuigwa kama Chuo kinachojenga na
kuimarisha kada ya Sheria.
“Chuo
hiki kweli ni kitovu na kisima cha elimu bora. Kimsingi, chuo kina uwezo wa
kujenga taaluma na kuwanoa wataalam mbalimbali wa Sheria wanaokwenda kusimamia
haki wakiwemo Mahakimu na watumishi wengine wa mahakama.” Alisema Dkt.
Ndumbaro.
Akizungumza
mara baada ya kukagua mazingira ya chuoni hapo yakiwemo mabweni, Mhe. Dkt.
Ndumbaro amebainisha kuwa Chuo hicho kimekuwa kikifanya kazi nzuri kwa kutoa mafunzo
mbalimbali elekezi na endelevu kwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania yakiwemo
mafunzo elekezi kwa Mahakimu wote mara wanapoajiriwa kujiunga kwa mara ya
kwanza na utumishi wa Mahakama kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutenda haki
kwa wote na kwa wakati kwa kuzingatia misingi ya sheria na uadilifu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Mheshimiwa Dkt. Gerald A. M. Ndika amesema Chuo kimekabidhiwa majukumu
ambayo ni kutoa mafunzo, kufanya tafiti na kutoa huduma za kitaalamu majukumu
ambayo Chuo kimemudu kuyatekeleza kwa ufanisi.
Tangu
kuanzishwa kwa Chuo hicho, mhimili wa Mahakama ndiyo mnufaika mkubwa wa zao la
kitaaluma la Chuo hicho kwani mhimili huo umeweza kuendeleza watumishi wake
pamoja na kuajiri Mahakimu na watumishi wengine kutoka katika Chuo hicho. Chuo
cha IJA pia kimekuwa kikiratibu na kufanya mafunzo endelevu ya kujengea uwezo
watumishi mbalimbali wa Mahakama.
Katika
ziara hiyo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro aliambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu na kupokelewa Uongozi wa Chuo
ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo na Jaji wa Mahakama ya
Rufani, Mheshimiwa Dkt. Gerald A. M. Ndika na Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe.
Dkt. Paul F. Kihwelo.
Comments
Post a Comment