Wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria washiriki maadhimisho ya siku ya Wanawake


 Watumishi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wakishangilia kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma. 

                            XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Wafanyakazi wanawake wa Wizara ya Katiba na Sheria wameadhimisha siku ya Wanawake Duniani Kwa kuungana na wanawake wengine kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi katika maadhimisho hayo kimkoa yaliyofanyika katika Wilaya ya Kondoa.

Maadhimisho hayo yamefanyika Machi 08, 2023 ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rosemary Senyamule.

Watumishi hao wameshiriki kwenye maandamano yaliyopokelewa na Mgeni Rasmi wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali.

Dkt. Senyamule wakati akiongea na watumishi wanawake kutoka ofisi mbalimbali amewaasa kujiamini na kuwa imara ili waweze kutimiza malengo yao bila kusubiri kusukumwa kwani uwezo wanao wa kufanya mambo makubwa kwa ajili ya jamii yao.

Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2023 yamebebea na kauli mbiu " ubunifu na mabadiliko ya teknolojia chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA