Waziri Mkuu azindua Mama Samia Legal Aid Campaign Dodoma
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (katikati), Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (kulia), Bi. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (kushoto) katika picha ya pamoja na sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwenye hafla ya uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign tarehe 27 Aprili, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku - WKS Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameizundua rasmi kampeni ya msaada wa kisheria inayoitwa Mama Samia Legal Aid Campaign kwa mkoa wa Dodoma Aprili 27, 2023 huku akiwataka watanzania kuitumia kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu, au vikundi vya watu ambao ama wanajihusisha na ukatili wa kijinsia hususan kwa watoto. Waziri Mkuu amesema kuwa kampeni hiyo itasaidia kuongeza uelewa wa sheria na upatikanaji haki, mifumo ya utoaji haki, masuala ya kisheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na taasisi za Serikali, Asasi za kiraia na Wadau wa Maendeleo katika ...