Mswada Sheria ya Ndoa Kuingia Bungeni


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na sehemu ya Menejimenti ya Wizara katika picha ya pamoja na Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake walipotembelea ofisi za Wizara Mtumba, Jijini Dodoma Aprili 5, 2023.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 Farida Khalfan & Lusajo Mwakabuku - WKS

 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake waliowakilisha mashirika takribani 400 yanayotetea haki za wanawake, wasichana na watoto nchini Tanzania, tarehe 05 Aprili, 2023 ofisini kwake, Mtumba Jijini Dodoma.

Kupitia kikao hicho Waziri ameeleza nia ya Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kupeleka mswada wa mabadiliko ya Sheria ya Ndoa, 1971 katika Bunge hili la bajeti, ili kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuolewa na kuoa kama ilivyoelekezwa na Mahakama.

Aidha, Wakurugenzi kutoka Jukwaa la Wakurugenzi Wanawake walitumia fursa hiyo kumhakikishia Waziri na ofisi yake ushirikiano katika kuhakikisha mchakato huo unapelekea kuwa na Sheria nzuri yenye mlengo wa kijinsia kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kwa watoto hasa watoto wa kike.

Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA