MAHABUSU WALALAMIKIA VITENDO VYA RUSHWA MANYARA
Timu ya wataalamu na uongozi wa gereza wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi hiyo ya kutoa msaada wa kisheria kwa watu walio vizuizini. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS MANYARA Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameuagiza Uongozi wa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Manyara pamoja na viongozi wa Jeshi la Polisi Mkoani humo kufanya uchunguzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mahabusu na Wafungwa wa gereza la Babati Mjini dhidi ya askari na watumishi wa vyombo hivyo vya haki ambapo katika nyakati tofauti wameonekana kutumia nafasi zao kudai rushwa kwa malengo ya kukwepesha haki. Tuhuma hizo zimetolewa tarehe 24/05/2023 wakati timu ya wataalam wanaoendesha Mama Samia Legal Aid Campaign ikiongozwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gek...