DKT NDUMBARO AKEMEA UKATILI WA KINJISIA KONDOA

        Mkazi wa Wilaya ya Kondoa akimweleza jambo Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro(hayupo pichani) Baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara ya kukagua maenedeleo ya Mama Samia legal aid Campain  katika Wilaya ya Kondoa tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma. 

 


   Wananchi wa Wilaya ya Kondoa wakiwa wamejitokeza kwenye viwanja vya soko kuu kumsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro alipokuwa alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu Mama Samia Legal Aid Campain  tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma. 


Mwananchi wa Wilaya ya Kondoa akimweleza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro mgogoro wa ardhi baada ya Waziri Ndumbaro kufanya ziara ya kukagua maenedeleo ya Mama Samia legal aid Campain katika wilaya ya Kondoa tarehe 6 mei 2023 jijini Dodoma 

              xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na George Mwayembe – WKS Kondoa

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damas Ndumbaro amekemea vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia unaojitokeza katika jamii zetu kwani licha ya kukiuka misingi ya haki za binadamu, vitendo hivi vinakwenda kinyuma na maadili ya katika jamii zetu zinazotutambulisha kama watanzania. Dkt ndumbaro ameyasema hayo alipokuwa   akito elimu ya sheria pamoja na msaada wa kisheria kwa wananchi wa Wilaya ya Kondoa na Chemba Mkoani Dodoma Tarehe 5 Mei, 2023.

Dkt ndumbaro ameyasema hayo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa Mama Samia Legal Aid Campaign kampeni inayolenga kutoa msaada wa elimu ya kisheria unaofanyika katika wilaya zote mkoani Dodoma tokea Aprili 28 mwaka huu katika wilayo zote za Dodoma.

Aidha, Waziri Ndumbaro amesema kuanzia sasa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku ya kutoa elimu ya sheria na msaada wa kisheria kwa wananchi.

 “Kwa hatua hii ya mwanzo tunaishia tarehe 7 may lakini kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuanzia sasa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi uongozi wa wilaya utashirikiana na wizara kutoa elimu elimu ya sheria na msaada wa sheria kwa wahitaji hususani wananchi wanyonge ambao wengi wako vijijini.” Alisema Mhe. Ndumbaro.

Mhe. Ndumbaro aliongeza kuwa Wilaya kwa kushirikiana na timu ya Wizara ya Katiba ya Sheria itakiwa ikitoa elimu na msaada wa sheria kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi katika kata itakayopangwa. “Tukimaliza tutaendelea kurudi na kurudi ili kila mtanzania popote alipo katika kona ya nchi hii lazima apate elimu ya sheria na apate msaada wa kisheria. Lengo letu ni kuwa baada ya miaka mitatu, kila kata na kila kijiji kiwe kimefikiwa na huduma hii na wananchi wote wafikiwe na huduma hii ambayo Rais Samia ameamua kuitoka kwa wananchi bila malipo.”

Vilevile Dk Ndumbaro alipongeza juhudi za serikali ya awamu ya sita akisema ndani ya miaka mwili ya uongozi wa Rais Samia kuna mambo makubwa yamefanyika katika sekta ya sheria ikiwemo kutekeleza kikamilifu Sheria ya Msaada wa Kisheria iliyotungwa na Bunge mwaka 2017.

 “Watanzania tuna deni la kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ammpe afya, uzima aendelee kututumikia na kujali, tuna deni la kupambana na wale wanaompinga mheshimiwa Rais na tuna ndeni la kuhakikisha tunaendelea na Rais huyu ifikapo mwaka 2025.”

Kampenzi hii katika mkoa wa Dodoma ilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Aprili 27 jijini Dodoma ambapo ndani ya siku sita tangu kuanza Kampeni hiyo, wananchi wa kata 10 za Wilaya ya Chemba wamefikiwa na huduma hii ambapo kwa Wilaya ya Kondoa wananchi zaidi ya 5,000 wamepata elimu na wengine kupewa msaada wa kisheria.







Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA