KAMPENI YA MAMA SAMIA YATATUA MGOGORO BEREGE.


 Mwenyekiti wa kijiji cha Berege ndugu Zebedayo Mchiwa akimshika mkono mwakilishi wa wananchi wa kijiji cha berege baada ya kupatanishwa na kumalizika kwa mgogoro uliotatuliwa na mafisa wanaotoa  msaada wa kisheria kwenye kampeni ya Mama Samia Legal Aid katika Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma.  



Wananchi wa kijiji cha Berege Kata ya Berege Wilaya ya Mpwapwa wakiwa wanasikiliza elimu ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid Campain ambayo inatolewa na wataalaam kutoka Wizara ya Katiba na Sheria. Kampeni hii imeanza tangu tarehe 28 aprili na kuhitimishwa tarehe 7 mei 2023. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na George Mwakyembe & Lusajo Mwakabuku – WKS  Mpwapwa. 

Mama Samia Legal Aid Campaign inayoendelea mkoani Dodoma imekuwa msaada mkubwa katika kutatua matatizo mbalimbali katika jamii mbali ya kutoa elimu ya kisheria, pamoja na msaada wa kisheria. Hilo limethibitika katika kikjiji cha Berege kata ya Berege Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma baada ya kampeni hii kuwakutanisha wanakijiji na mwenyekiti wao ambapo kwa takribani miaka mitatu hapakuwa na mahusiano mazuri hali iliyopelekea kushindwa kufanyika kwa vikao vya maendeleo katika Kijiji hicho.

Akiongea mbele ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na wataalamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja washirika wa azaki zisizo za kiserikali, mwenyekiti wa Kijiji hicho bwana Zebedayo Mchiwa alishukuru kwa ujio wa kampeni hii kwani umeweza kutibu mgogoro huo ambao ulipelekea kutoweka kwa hali ya amani na maelewano kati ya uongozi na wanakijiji.

“Kumekuwepo na tofauti kubwa zilizopelekea migongano kati ya mwakilishi wa wananchi na mimi lakini kwa kuwa wote tupo hapa kwa ajili ya kuhudumia wananchi na mimi ni kiongozi, nakubali kujishusha ili tuzike tofauti zetu kuanznia leo ili tuweze kuendelea kufanya kazi kwa pamoja zenye tija kwa wananchi wet badala ya kuendekeza tofauti zetu”. Alisema bwana Mchiwa.

Mgogoro huo umesababisha kutokuwepo kwa vikao vya kijiji kwa takribani miaka mitatu hatimaye umefikia kikomo baada pande zote mbili zilizokuwa zinapingana kukubali kumaliza tofauti zao na kutanguliza maendeleo ya nchi mbele hali ambayo imeshuhudiwa wataalamu wanaotoa msaada na elimu ya kisheria waliofika katika Kijiji hicho.

Baadaya pande zote mbili kukubalina na mwenyekiti wa kijiji emetangaza mkutano wa kijiji kuwa utakuwa siku ya jumatano tarehe 10 mei 2023 kujadili maendeleo ya kijiji. Mwenyekiti wa kijiji hicho ndugu Sila Zebedayo Mchiwa ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuwaletea kampeni ya msaada wa kisheria pamoja na elimu ya sheria kwani wamejifunza mengi pamoja na kupata uelewa mpana wa masauala ya sheria.

“hii ni fursa nzuri sana kwa wananchi wangu wa kata ya Berege kuweza kuyafahamu mambo mbalimbali yanayohusiana na sheria hivyo ni vyema mkaitumia vizuri nafasi hii katika kupata elimu lakini pia hata itatusaidia katika kutatua migogoro midogomidogo ambayo si lazima ifike mahakamani”.  Alimalizia bwana Mchiwa.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA