MKUTANO WA 77 WA HAKI ZA BINADAMU NA WATU KUFANYIKA JIJINI ARUSHA

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) akiongoza kikao kazi cha maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu . tarehe 28 Juni 2023 Jijini Arusha XXXXXXXXXXXXXXXXXXX William Mabusi - WKS Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) ameongoza timu ya Wizara kwenye Kikao Kazi kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa 77 wa Haki za Binadamu na Watu utakaofanyika hapa nchini mnamo tarehe 20 Oktoba mpaka 9 Novemba, 2023 mkoani Arusha na kuagiza usimamizi mzuri wa maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo. Kikao Kazi hicho kimefanyika Jijini Arusha tarehe 28 Juni, 2023 na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Mary Makondo, Mwenyeji Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. John Mongella, ndugu Steven Zelothe Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha miongo...