MADAWATI YA JINSIA SI KWA AJILI YA WANAWAKE PEKEE - MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johary Shamizi ( wa tatu kulia ) katikati kwenye picha ya pamoja na timu ya Mama Samia Legal Aid Campain (MSLAC) walipofika ofisini kwake kujitambulisha tarehe 12 juni 2023.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na William Mabusi – WKS Shinyanga
Mkuu wa
Wilaya ya Shinyanga Bi. Johary Shamizi amesema moja ya sababu za wanaume
kushindwa kujitokeza kutoa malalamiko yao kwenye dawati la jinsia ni kwa kuwa
hawapendi malalamiko yao kusikilizwa na mwanamke hali inayofanya kujikuta
wanakosa msaada hata pale wanapouhitaji.
Bi. Shamizi
ameyasema hayo tarehe 12 Juni, 2023 alipokutana na kuzungumza na timu ya
wataalam wa MSLAC waliofika ofisini kwake kujitambulisha ambapo pamoja na mambo
mengine alipongeza jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuona
wananchi wengi wa hali ya chini wanapata elimu ya sheria na kuwaagiza wananchi
hususan wanaume kujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyo kupata elimu juu ya
ukatili wa kijinsia kwani wapo wanaume wanaokumbana na ukatili wa kijinsia.
Bi. Shamizi
amesema “kampeni hii iwasaidie watu wenye shida ya kweli, wanaume nao wapewe
elimu kwani ukatili wa kijinsia ni pande zote.”
Akiwatoa
hofu wanaume ya kusikilizwa na akina mama kwenye Madawati ya Kijinsia, Afande
Monica Venance Sehere kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Halmashauri ya
Shinyanga amesema Madawati hayo sasa yana akina baba wanaosikiliza changamoto
za wanaume.
“Kesi
nyingi zinazoripotiwa ni kuhusu wanawake na watoto na hii inasababisha Dawati
hilo kuonekana ni la akina mama na watoto kumbe hata wababa wanahusika
isipokuwa akina baba hawaripoti malalamiko yao.” alisema Afande Monica.
Kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Masengwa Diwani wa kata hiyo Mhe.
Nicodemas Simon aliwataka wananchi kutumia uelewa walioupata kwenye elimu ya
sheria inayotolewa kuacha mila potofu zinaosabisha ukatili wa kijinsia na
uvunjifu wa amani katika jamii na kuachana na taratibu zisizo rasmi za kumaliza
kesi za unyanyasaji wa kijinsia na mimba za utotoni kwa makubaliano ya
kulipishana ng’ombe kwa waliotenda vitendo hivyo kitu ambacho ni kinyume na
taratibu kwani watuhumiwa hao wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mkoa wa
Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayoongoza katika vitendo vya ukatili wa
kijinsia. Mkuu wa Mkoa huo Bi. Christina Mndeme wakati anazindua kampeni hiyo
mkoani kwake alisema anamatumaini makubwa kwamba kampeni hiyo itasaidia
kupunguza kama siyo kumaliza kabisa vitendo hivyo.
Comments
Post a Comment