MKUU WA WILAYA AWANYOOSHEA KIDOLE WATUMISHI WA ARDHI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Musa Samizi akipokea mrejesho wa utekekelezaji wa Mama Samia Legal Aid Campain iliyokuwa inafanyika kwenye yake . tarehe 21 Juni 2023.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na William Mabusi – WKS Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Johari Musa Samizi
amewataka watumishi wa ardhi kufanya kazi kwa kufuata haki na taratibu za kazi
wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku katika kuwahudumua wananchi ili
kuepuka kusababisha migogoro ya ardhi nchini.
Bi. Samizi ameyasema hayo wakati timu zilizokuwa
zinatekeleza kampeni ya kitaifa ya Mama Samia Legal Aid Campaign kwenye
Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga zilipofika ofisini
kwake tarehe 21 Juni, 2023 kutoa mrejesho wa utekelezaji wa kampeni hiyo
iliyokuwa inatekelezwa mkoani humo kwa siku kumi kuanzia tarehe 11 hadi 20 Juni
2023.
Mtumishi anafanya anachojua na siyo kwamba hajui
anachofanya, anajua kabisa hapa nachakachua na hapa sitendi haki lakini
anafanya tu, mwananchi mnyonge ndiye anayeumizwa zaidi labda mwananchi huyo awe
mnyonge na awe mbishi kweli kweli. Nawaasa watumishi wenzangu tuwatendee haki
wananchi kwani wao ndio wanafanya twende kazini, wasipokuwepo hatuna kazi.”
Alisema Bi Samizi.
Katika siku kumi za kutekeleza kampeni hiyo katika Mkoa
wa Shinyanga ambapo yeye mwenyewe alishiriki kwa nyakati tofauti, elimu ya
sheria imetolewa, wananchi wamepewa huduma ya msaada wa kisheria na baadhi ya
migogoro kupatiwa ufumbuzi.
Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amesema, “Kampeni hii
imetupunguzia kazi, migogoro mingi imetatuliwa na hiyo mingine inayotakiwa
kufuatiliwa tutaifuatilia, maeneo mengi nilikuwa nikienda nakutana na migogoro
tu lakini kwa kampeni hii tumefanya jambo.”
Ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata elimu ya
sheria na huduma ya msaada wa sheria hata baada ya kampeni hiyo kumalizika
wilayani mwake, Bi. Samizi amaesema atajipanga na Wataalam wake katika kila
ziara atakayofanya kwenye Kata ataambatana nao ili watoe elimu kwanza kabla ya
yeye kuhutubia.
Akiongelea mamlaka iliyonayo Serikali za Vijiji kuhusu
ardhi Bi. Samizi amesema, “Serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya ardhi,
pale inapotokea viongozi hao wametoa ardhi ya Kijiji kwa sababu yoyote ile
watoe taarifa kwa wananchi wao ili kuepusha migogoro.
Awali,
timu ya MSLAC iliyokuwa inatekeleza kampeni hiyo kwenye Halmashauri ya Wilaya
ya Shinyanga ilikutana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga Dkt.
Nuru Yunge kumpa mrejesho wa kampeni hiyo huku ikilalamikia mwitikio mdogo wa
akina mama kwenye mikutano ya hadhara, changamoto ambayo amesema itafanyiwa
kazi kwenye matukio mengine yatakayofuata.
Comments
Post a Comment