ONGEZENI JUHUDI KATIKA UTOAJI ELIMU YA SHERIA KWA UMMA: GEKUL
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Pauline Gekul akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha sheria hawapo picha tarehe 22 Juni 2023 jijini Dododma .
XXXXXXXXXXXXXXXXX
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Pauline Gekul amewataka watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria
kuongeza juhudi katika suala la utoaji elimu kwa umma kuhusiana na
masuala mbalimbali ya kisheria ili jamii iweze kuzitambua Sheria zilizopo
nchini na kuwasaidia kuzitumia hususan pale ambapo wanapotaka kufahamu haki zao
juu ya jambo husika.
"Kiu
kubwa ya jamii ipo kwenye elimu, sheria tunazo nyingi sana zimetungwa lakini
jamii zetu haizifahamu sheria hizo na wengi wanateseka kupata haki zao kupitia
sheria kwasababu hawana elimu ya kutosha ya kuzijua sheria hizo."
Mhe. Gekul
amebainisha hayo wakati akizungumza na Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria
Tanzania alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea Tume hiyo iliyofanyika
tarehe 22 Juni, 2023 Jijini Dodoma.
Naibu Waziri
Gekul yupo katika ziara ya kutembelea Taasisi mbalimbali zilizopo ndani
ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa lengo la kufahamiana, kufahamu
majukumu yao, mafanikio na changamoto mbalimbali zinazoikumba taasisi hizo.
Aidha, Naibu
Waziri amewataka watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria kutoa elimu ya sheria
kwa umma kupitia nyanja mbalimbali zikiwemo Vyombo vya Habari, Mitandao ya
Kijamii na Semina mbalimbali ili kuwasaidia wananchi kuzijua sheria za nchi
na kupata haki zao kupitia sheria hizo.
Comments
Post a Comment