Tufanye kazi na kushiriki kwenye Michezo: Dkt. Ndumbaro
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas
Ndumbaro akipokea medal ambazo Wizara ilishinda kwenye Marathon ya miaka 60 ya
JKT, tarehe 27 Juni, 2023.
Watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa kwenye hafla ya kuwapongeza watumishi walioshiriki kwenye marathon ya miaka 60 ya JKT, tarehe 27 Juni, 2023.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na William Mabusi - WKS
Waziri wa Katiba na
Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesisitiza watumishi wa Wizara hiyo
pamoja na kutekeleza majukumu yao lakini pia washiriki kwenye michezo kwani michezo
huimarisha afya.
Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo tarehe 27 Juni, 2023 wakati wa
hafla ya kuwapongeza watumishi walioshiriki kwenye marathon ya Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) kufikisha miaka 60 iliyofanyika tarehe 25 Juni, 2023 ambapo Wizara
ilishiriki na kuwa miongoni mwa Wizara zilizopata Medali, Mgeni Rasmi kwenye
marathon hiyo alikuwa Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Aidha, Waziri alisisitiza watumishi kufanya kazi kwa
kushirikiana na kutekeleza majukumu kwa wakati, “tumia kipaji chako katika
kutimiza majukumu yako kwa dhati kabisa. Hatuna sababu za kuchelewesha kazi,
unalipwa kwa sababu unafanya kazi na si ulipwe kwa sababu umeajiriwa.” Alisema
Dkt. Ndumbaro huku akiwataka watumishi hao kujiandaa na jukumu kubwa lililo
mbele yao la Katiba Mpya.
Akiongelea kuhusu ushiriki wa michezo, Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bi. Mary Makondo alisema Wizara itaendelea kushiriki katika michezo
mbalimbali na ana matarajio makubwa kuhusu ushiriki na kufanya vizuri kwa
Wizara ya Katiba na Sheria kwenye michezo ijayo ya SHIMIWI.
Comments
Post a Comment