Wizara imejipanga kuendelea kujenga Mahakama nchini - Pauline Gekul.


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh.Pauline Gekul aitoa ufafanuzi wa swali aliloulizwa  na mbunge wa kigoma kusini mheshimiwa Nashon Bindyanguze leo tarehe 20 juni 2023  Bungeni Dododma.

                                                   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na. George Mwakyembe. WKS – Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema Wizara imejipanga kundelea na ujenzi wa Mahakama nchini kwa mwaka wa bajeti 2023/2024 na tayari Wizara imejipanga kujenga zaidi ya mahakama 60.

Mheshimiwa Gekul amesayema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kigoma mheshimiwa Nashoni Bindyanguze mbunge wa Kigoma Kusini. Mheshimiwa Gekul amesema kwa mwaka wa bajeti 2024/2025 Wizara itajenga Mahakama ya Mwanzo katika eneo la Mgambo ambalo ndiyo makao makuu ya Tarafa ya Buhingu.

Naye mbunge wa Arusha mjini Mhe. Mrisho Gambo aliuliza swali la nyongeza kwa mheshimiwa Naibu Waziri Gekul kutaka Kujua ujenzi wa mahakama ya mwanzo katika kata ya Terati. Mheshimiwa Gekul amemhakikishia kuwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 ujenzi wa mahakama tayari kata ya Terati ni kata mojawapo ambayo ujenzi huo utajengwa.  

Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Manyara Mhe. Asia Halamga aliuliza swali kutaka kujua ujenzi wa mahakama eneo la mijingu Mkoani Manyara. Mhe. Naibu Waziri Gekul amemtoa wasiwasi na kwamba hilo eneo tayari liko kwenye mpango wa ujenzi wa mahakama kwa mwaka fedha unaokuja.

Naye mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Shinyanga  Mheshimiwa Christine Mzava ameomba Wizara kufanya ukarabati  wa mahakama za kata ya Usanda na Samuye kwani zimejengwa tokea enzi za mkoloni, Mheshimiwa Gekul  amemhakikishia  kuwa mahakama hizo zitafanyiwa ukarabati .  


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA