Wizara ya Katiba na Sheria yakutana na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola


 Wawakilishi kutoka RITA wakifafanua jambo kuhusu namna taasisi ya RITA inavyofanya kazi wakati wa kikao na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola. Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma

 Mwenyekiti wa Sekretarieti ya tathimini kutoka Jumuiya ya Madola Bi. Evelyn Pedersen (wa nne kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya watalaamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake, Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma.


Bi. Evelyn Pedersen (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma Ndg. Abdulrahman Mshamu pamoja na watalaam wengine kutoka Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake, Tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma.

George Mwakyembe- WKS

Wizara ya Katiba na Sheria wamefanya kikao na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola. Katika kikao hicho ambacho kimeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma Ndg. Abdulrahman Mshamu akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizra ya Katiba na Sheria.   

Katika kikao hicho ambacho kimefanyika leo tarehe 28 Juni 2023 Jijini Dodoma. Sekretarieti hiyo imeipongeza Tanzania kwa kuendelea kuwa daraja la kwanza katika kutekeleza Haki za Binadamu. Hizi juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Haki za Binadamu zinatekelezwa pamoja na kulindwa.

Akiongea kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Sekretarieti Bi. Evelyn Pedersen amesema “kwa thatmini ambayo tumekuwa tukifanya kwa nchi za Jumuiya ya Madaola tunategemea kujengeana uwezo baina ya Tanzania na nchi wanajumuiya ya Madola katika masuala mbalimbali yahusuyo jamii zetu ni vyema tukaangalia wapi tunatakiwa kupafanyia kazi ili tuweze kushirikiana.”

Mwenyekiti huyo amesema “Katika nchi wanajumuiya ya Madola, Tanzania ni nchi ya kuigwa hasa katika kuimarisha amani, umoja na utulivu wa wananchi wake na hii inatupelekea kupanga kufanya kikao cha Mawaziri wa nchi za Jumuiya za Madola hapa nchini ifikapo mwakani ambacho kitajadili masuala mbalimbali yahusuyo nchi zetu” 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA