Tusiwe Chanzo cha Migogoro Tutatue Kero za Wananchi – Gekul
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akiongea na wananchi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akisikiliza malalamiko ya Ndg. Victory Luena mkazi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akionge na wananchi wa kijiji cha Liuli kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipokuwa akirejea kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe - WKS Nyasa . Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) amefanya ziara na kukutana na wananchi wa Kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma tarehe 30 Julai, 2023. Akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya kampeni ya Mama Samia Msaada wa ...