Bi. Makondo afanya mazungumzo na Ujumbe wa Ubalozi wa Marekani
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiongea jambo alipokutana na kufanya
mazungumzo na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Marekani nchini, tarehe 17 Julai, 2023
Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo
(kulia), kwenye picha ya pamoja na Wageni wake kutoka Ubalozi wa Marekani Balozi
Michele Sison (kushoto) na Prof. Sarah Cleveland (katikati), 17 Julai, 2023.
Ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akiwa na Menejimenti ya Wizara hiyo amekutana na kufanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Marekani nchini ulioongozwa na Balozi Michele Sison kwenye Ofisi za Wizara Mtumba Jijini Dodoma tarehe 17 Julai, 2023.
Katika
mazungumzo yao pande zote mbili zimepongeza ushirikiano uliopo kati ya Tanzania
na Marekani kwenye nyanja mbalimbali na kutaka ushirikiano huo uendelee pia
kwenye sekta ya sheria kwa kuwajengea uwezo wa wataalamu wa ndani katika
masuala ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala, uandishi wa mikataba na
kufanya tafiti kwenye uandishi wa mikataba ya kimataifa.
Aidha, Ujumbe huo umepongeza jitihada zinazofanywa na Serikali
ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye
maboresho ya sheria mbalimbali nchini kwa manufaa ya watanzania.
Comments
Post a Comment