MAFUNZO YA ULINZI KWA WATOA TAARIFA NA MASHAHIDI YAFANYIKA DODOMA.
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bw. Khalist Luanda akifafanua maada kuhusu sheria na kanuni za kumlinda mtoa taarifa na ushahidi kwa maafisa kutoka taasisi za haki jinai leo tarehe 30 Juni 2023 jijini Dodoma.
Maafisa kutoka katika taasisi za haki jinai wakiwa wanasikiliza maada kutoka iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Khalist Luanda leo tarehe 30 Juni 2023. Jijini Dododoma.
Na George Mwakyembe – WKS
Wizara ya Katiba na Sheria imefanya mafunzo juu ya
Sheria na Kanuni za watoa taarifa na mashahidi kwa Maafisa mbalimbali kutoka
taasisi za haki jinai tarehe 30 Juni, 2023 Jijini Dodoma yenye lengo la
kuwajengea uwezo wa kumlinda mtoa taarifa na ushahidi wakati
wa kutekeleza majukumu ya Serikali.
Akiwasilisha mada, Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na
Ufuatiliaji Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Khalist Luanda amesema
“Sheria ya kumlinda mtoa taarifa na ushahidi lazima izingatiwe kwani ni Sheria
ambayo itasaidia kupunguza masula ya uhalifu kwa sababu taarifa zao zitakuwa
zinatolewa na kufanyiwa kazi lakini kanuni hizi zinamlinda mtoa taarifa.
Mnaagizwa kuzitekeleza na kuzifuata ipasavyo kwa sababu ninyi ndiyo wapokeaji
taarifa za haki jinai.”
Aidha, Bw. Luanda amesema changamoto kubwa
inayojitokeza kwenye Sheria hiyo ni wapokeaji taarifa kutotunza siri baada ya
kupokea taarifa kitu ambacho kimekuwa changamoto sana kwani inaleta udhaifu wa
namna ya kukabiliana na wahalifu baada ya kupokea taarifa. Kwa Kanuni na Sheria
hii inaruhusu utanzaji wa siri ili mtoaji wa taarifa alindwe.
Mada hiyo ya kanuni inayoitwa The
Whistleblower and Witness Protection Regulations, 2023 inaelezea
namna ya kulinda usalama wa mtu anayetoa taarifa za uhalifu na kanuni hiyo inasomwa
pamoja na sheria ya The Whistleblower and Witness Protection Act
(Cap.446).
Akichangia kwenye mafunzo hayo ndugu John Kidando
kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema sheria hiyo ni muhimu sana
kwa sababu inamlinda na kumpa haki mtu anayetoa taarifa, iwapo mtu aliyetoa
taarifa atatakiwa kupewa zawadi baada ya kutoa taarifa basi atatakiwa kupewa
kwa kulindwa pasipo kutoa taarifa zake.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na maafisa kutoka Ofisi ya
Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Rais TAMISEMI,
pamoja na Maafisa wa Polisi kutoka mkoa wa Dodoma ambao wote ni walengwa
wakubwa katika kupokea taarifa mbalimbali za uhalifu na zenye manufaa kwa Taifa.
Comments
Post a Comment