SHERIA ZOTE KUPATIKANA KWENYE MIFUMO YA KIDIGITALI – Dkt Ndumbaro.


        Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro akiongea wageni rasmi kwenye (hawapo pichani) kwenye warsha ya utiaji saini mikataba ya kuweka mifumo ya sheria kidigital leo tarehe 13 Julai 2023 Jijini Dodoma.

Majaji wa Mahakama ya Rufaa  wakiwa wanasikiliza hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro alipokuwa akizindua warsha ya upatikanaji wa Sheria kidigitali liliofanyika tarehe 13 Julai Jijini Dodoma.  


Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Ndg. Griffin Mwakapeje akionyesha Mkataba wa makubaliano ya kuhakikisha sheria zote zinapatika kidigital. Mikataba hiyo imesiniwa leo tarehe 13 Julai 2023 Jijini Dodoma.

  Majaji wa Mahakama ya Rufaa wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (Katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo (wa Kwanza Kulia) waliokaa.

                       XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na George Mwakyembe, WKS

Waziri wa Katika na Sheria Dkt Damas Ndumbaro ameshuhudia utiaji saini wa mikataba miwili na taasisi ya African Legal Information Institute (AfricanLII) ambayo imelenga kuhakikisha Sheria zote na maamuzi ya Mahakama kupatikana kidigitali. Hayo yamefanyika leo tarehe 13 Julai 2023 jijini Dodoma. 

Mikataba hiyo  imeseiniwa kati ya AfricanLII na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na AfricanL II na Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiliaji saini wa mikataba hiyo na kufungua warsha ya upatikanaji endelevu wa kidigitali kwa sheria za Tanzania, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Damas Ndumbaro “amesema mradi huo utahikikisha Sheria zote za Tanzania kubwa na Sheria ndogo zinapatikana kwenye mifumo ya kidigitali”

Dkt Ndumbaro amesema “Hili haliishii kwenye sheria bali tu tunakwenda mpaka kwenye maamuzi ya Mahakama, falsafa ya Sheria inasema kutojua Sheria si utetezi. Hivyo Serikali imeamua kutekeleza kwa vitendo kwa kuhakikisha Sheria na maamuzi yanayotolewa na Mahakama zinapatikana kwa urahisi mahali popote pale kwa njia ya kidigitali.”

Aidha, Dk Ndumbaro amesema hatua hiyo itasaidia kukuza upatikanaji wa haki kwa wananchi kirahisi zaidi lakini pia italeta ushirikiano na Taasisi na wadau wa Sheria wakiwemo wanaofanya tafiti pamoja na walimu wa vyuo vikuu.

“Pia itasaidia wananchi na taasisi za serikali ambazo zinatumia sheria mbalimbali kuweza kuzipata kirahisi, ule muda wa kuondoka na kwenda maktaba ukatafute kitabu cha sheria uisome sasa umepitwa, tunatumia mapinduzi ya kitekinolojia kuhakikisha tunapeleka haki kirahisi na kwa wepesi kwa kila mtanzania.”

Vilevile Dkt Ndumbaro amesema “Serikali chini ya usimamizi wa Wizara ya Katiba na Sheria imekubali mfumo wa kidijitali kama mkakati wa kimsingi wa kurahisisha shughuli za serikali, kuimarisha uwazi, na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma” “Upatikanaji wa haki kwa Watanzania wote ni jambo la lazima katika Wizara ya Katiba na Sheria na miaka michache iliyopita, Wizara iliweka juhudi za ziada ili kuimarisha upatikanaji wa haki kwa wanawake na wasichana nchini Tanzania.

Aidha Dkt Ndumbaro amesema “tunafanya hivyo ili Sheria zetu zipatikane kwa urahisi na

hili  itatuwawezesha watanzania wote  wanawake na wasichana kufikia huduma hiyo ili kudai haki zao na kutafuta suluhu.” Kwa kuona umuhimu wa hilo tayari Serikali imeanzisha Kampeni ya Mama Samia msaada wa kisheria ambayo tayari imefanyika kwenye mikoa ya Dodoma, Manyara na Shinyanga na kuwa wiki ijayo utazinduliwa  rasmi na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango katika  Mkoa  wa Ruvuma.

Dkt Ndumbaro amesema pia “Serikali imefikia uamuzi wa kutafsiri Sheria kwenda kwenye lugha ya Kiswahili ili zieleweke na watanzania wote na kuwataka wadau wanaotafsiri kuhakikisha wanatoa tafsiri zilizo sahihi.

Akiongea kwenye warsha hilo naye mwakilishi wa GIZ, Bw, Richard Shaba amesema “hatua hiyo itasaidia itawarahishia Serikali katika kutoa maamuzi na pia itaweka urahisi kwa watafiti wa Sheria na walimu wa sheria.

Katika warsha hiyo viongozi mbalimbali wamehudhuria akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi, Mary Makondo.  




Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA