TUPINGE NDOA ZA UTOTONI NI ADUI WA NDOTO ZA MABINTI WETU.
Mkurugenzi msaidizi wa Haki za Binadamu Ndg. Richard Kilanga akiongea na Wananchi wa kijiji cha Mtipwili kuhusu ukatili wa kijinsia, miradhi, migogoro ya ardhi pamoja na ndoa za utotoni wakati wa utekelezaji wa Mama Samia Leagal Aid Campain Wilaya Nyasa Mkoa wa Ruvuma.
Na, George Mwakyembe – Nyasa
Mkurugenzi
Msaidizi wa idara ya Haki za binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Ndg.
Richard Kilanga amesema ni lazima jamii zetu ziungane kupinga vikali suala ukatili
wa kijinsia.
Hayo
amesema jana alipokuwa akiongea na wananchi wa kata ya Mtipwili Wilaya ya Nyasa
Mkoani Ruvuma. Ndg Kilanga amesema “ifike wakati sasa jamiii yetu tuungane
kupinga na kutokomeza suala la ndoa za utotoni, watoto wetu wanapewa mimba na
watu ambao tunawajua lakini baadhi yetu kwenye jamii zetu hawatoi ushirikiano pale mtoto anapopata
mimba kwa kuhofia au kupewa chochote kitu. Hili suala haliwezekani lazima
tisimame kwa pamoja na kukemea vitendo hivi kwa nguvu ya pamoja.
Aidha
Ndg Kilanga amesema “unapoona mwanafunzi au mtoto kapewa mimba basi toa taarifa
mapema kwa vyombo husika ikiwemo polisi ili hatua za kisheria zichukuriwe
haraka sana. Ndoto za watoto wetu lazima zitimie bila kukatishwa.
Akiongea
na wananchi wa kata ya Mtipwili kijiji cha Malini Bw. Kilanga amesema katika
wilaya ya Nyasa ndoa za utotoni ni tatizo kubwa sana lakini wananchi wamekuwa
wakilifumbia macho, hili sula halikubaliki kabisa, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania amekuwa mstari wa mbele kukemea vitendo hivi vya ukatili wa
kijinsia ikiwemo ubakaji, ulawiti pamoja na
vitendo vyote ambavyo ni ukatili wa kijinsia ndiyo maana Mheshimiwa Rais
wetu Mama Samia Suluhu Hassan katutuma
kukemea pamoja na kutoa elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia na ndoa za utotoni pamoja
na kutatua migogoro ya ardhi ambayo pia imekuwa kero kubwa sana katika jamii
zetu.
Kampeni
ya Mama Samia Legal Aid inaendelea baada ya kuzuduliwa na Makamu wa Rais Dkt
Philip Mpango tarehe 22 Julai Mkoani Ruvuma. Kampeni hiyo ambayo inafanyika katika
Wilaya zote za Mkoa Ruvuma imekuwa msaada mkubwa sana kwa jamii zetu katika kutatua matatizo
mbalimbali yanayowakabili wananchi. Kampeni ya Mama Samial Legal Aid kwa Mkoa
wa Ruvuma itafikia tamati tarehe 2 agosti 2023.
Comments
Post a Comment