Tusiwe Chanzo cha Migogoro Tutatue Kero za Wananchi – Gekul

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akiongea na wananchi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akisikiliza malalamiko ya Ndg. Victory Luena mkazi wa Kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipotembelea na kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023.


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) akionge na wananchi wa kijiji cha Liuli kata ya Liuli Wilayani Nyasa alipokuwa akirejea kukagua utekelezaji wa Kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria tarehe 29 Julai 2023

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na George Mwakyembe - WKS Nyasa.  

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) amefanya ziara na kukutana na wananchi wa Kata ya Liuli Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma tarehe 30 Julai, 2023.

Akiwa katika ziara hiyo ya kukagua maendeleo ya kampeni ya Mama Samia Msaada wa Kisheria inayoendelea mkoani Ruvuma Mhe. Gekul amefika katika kijiji cha Liuli na kuongea na Wananchi wa Kata hiyo pamoja na kupokea kero mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao.

Mhe. Gekul amesema “Wenyeviti na Watendaji tusiwe chanzo cha migogoro, tunatakiwa kutatua kero, na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi. Tumekuwa tukipokea malalamiko mengi ya wananchi wakilalamika kuwa baadhi yenu mnawanyanyasa wananchi kwa kutokuwatendea haki katika majukumu yenu.”

Ameyasema hayo baada ya wananchi wa kata hiyo kutoa malalamiko kuhusu kupokonywa mashamba na Mwenyekiti wa kijiji cha Nkarachi Bw. Ezekiel Haule. Katika malalmiko hayo ndugu Victory Luena alisema Mwenyekiti huyo amekuwa akichukua mashamba na kupanda miti aina ya mitiki pasipo kutoa fidia kwa wenye mashamba hali ambayo   wananchi wa kijiji cha Liuli kudai fidia kwani mashamba hayo wamekuwa wakiyamiliki kwa muda mrefu sana.

Mhe. Gekul aliwaambia Mwenyekiti na Mtendaji kuhakikisha mgogoro huo unakwisha pamoja na mwenye haki kupewe haki yake. Aidha Mhe. Gekul alisisitiza suala zima la utawala bora ili kuondoa migogoro isiyo na tija na kuondoa amani kwa wananchi.

Akiongea na wananchi Mhe. Gekul alisema “Mtendaji na Mwenyekiti lazima kuwashirikisha wananchi katika masuala yote yanayohusu maendeleo ya Kijiji, hii ndiyo dhana nzuri ya utawala bora. Ni vyema wananchi kujua Serikali yao inafanya mradi gani pasipo kufichwa fichwa na pamoja na kupata stahiki zao.”

Kampeni ya Mama Samia msaada wa sheria ipo mkoani Ruvuma tangu kuzinduliwa kwake tarehe 22 Julai, 2023 na kumalizika tarehe 02 Agosti 2023.

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA