MAHAKAMA KUENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI – MHE GEKUL

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akijibu maswali bungeni leo tarehe 30 Agosti 2023 . Dodoma. Na. George Mwakyembe - WKS DODOMA. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameeleza kuwa Mahakama inaendelea na mpango wa kujenga ofisi za Mahakama nchini kote na kwamba hadi sasa ofisi 18 za Mahakama za Wilaya zimeshajengwa na Mahakama za Mwanzo ni 71. Mahakama hizi zinajengwa kwa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 Mhe. Gekul ameyasema hayo leo tarehe 30 Agosti 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini Mhe, Daimu Idd Mpakate ambaye aliuliza lini Mahakama itajenga Mahakama za mwanzo katika Tarafa ya Nalasi, Lukumbule, pamoja na Tarafa ya Namasakata. Pia, Mhe. Gekul amefafanua kuwa tayari Mahakama ya mwanzo ya Nalasi inajengwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa mahakama 71 za mwazo ambazo zitajengwa nchi nzima na tayari mshauri elekezi ameanza kazi na ujenzi u...