DKT NDUMBARO AFUNGUA KIKAO CHA MAJADILIANO CHA MCHAKATO WA WA KATIBA MPYA
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.
Damasi Ndumbaro akiongea kwenye kikao
cha Majadiliano ya Katiba mpya na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kilichofanyika kwenye ukumbi Hyatt Regency
leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam .
Katibu Mkuu wa Wizara Katiba na
Sheria Bi. Mary makondo akiongea kwenye
kikao cha Majadiliano ya Katiba
mpya na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya
Katiba kilichofanyika kwenye ukumbi
Hyatt Regency leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam .
Makamu wa kwanza wa Zanzibar wa
Rais wa Serkali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Othamn Masoud Othaman akiwa katika
picha ya pamoja na Mawaziri wakuu
wataafu , pamoja na meza kuu (
waliosimama ) kwenye kikao Majadiliano
ya Katiba mpya na Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kilichofanyika kwenye ukumbi Hyatt Regency
leo tarehe 28 Agosti Jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro ameongoza Kikao cha Mawaziri wa Sheria na Wanasheria Wakuu wa Serikali Wastaafu na waliopo Madarakani kuhusu Majadiliano ya Mchakato wa katiba Mpya pamoja na Mkakati wa Elimu ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977
Akizungumza wakati akifungua kikao hicho tarehe 28 Agosti 2023 Jijini Dar es salaam Dkt Ndumbaro amesema lengo la kikao hicho kilikuwa ni kujadili mchakato wa katiba mpya pendekezwa ulioanza 2014 ambao bado haujafikia muafaka.
Dkt Ndumbaro ameongeza kuwa kikao hicho kimelenga kuongeza uelewa na kutoa elimu juu ya Mwenendo wa Mchakato wa Katiba mpya.
"Wizara kwa kutambua baadhi ya wananchi kudai Katiba mpya, uwepo wa Tume huru ya uchaguzi na Utawala unaozingatia Haki za Msingi za Binadamu na mambo mengine mengi ambayo yanahusisha shughuli za kimaendeleo, siasa na Katiba ya nchi. Kutokana na kuongezeka kwa hoja hizo na viashiria vya jamii kutofahamu haki za kikatiba, baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi, kushindwa kuheshimu utawala wa sheria na kutokujua wajibu wao kwa Taifa, hali inayopelekea kuwepo kwa mahitaji ya kuweka muongozo wa utoaji wa elimu ya Katiba katika masuala ya Haki za Binadamu na Haki na wajibu kwa jamii ya watanzania katika ngazi zote za kiutawala" amesema Waziri Dkt. Ndumbaro.
Dkt Ndumbaro alifafanua baadhi ya majukumu ya Wizara kwenye kikao hicho kuwa ni Kuratibu mchakato wa Katiba ya Mwaka 1977 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mawaziri wastaafu wanasheria na wale waliopo madarakani kupata mrengo mmoja uliokusudiwa
"Nimefungua kikao hiki Leo ili
kupitia kikao hiki tupate maoni yenu kwa upande wa Zanzibar na Tanzania bara
kufahamu wapi kulitakiwa kufanyiwa marekebisho katiba ya 1977 " Ameongeza
Dkt. Ndumbaro.
Comments
Post a Comment