Dkt. Ndumbaro Aongoza Kikao cha Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.


Bi. Mary Makondo Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria akikaribisha wajumbe kwenye Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023.


Mhe. Dkt. Damasi Ndumbaro akiongoza Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023.

Bw. Abdulrahman Mshamu Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma akitoa wasilisho la mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kwenye Kikao Kazi kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023.

 

Bw. Griffin Mwakapeje Katibu Mtendaji wa Tume ya Kubadili Sheria akichangia kwenye Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023.

Na. William Mabusi. WKS

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameongoza Kikao Kazi cha kujadili mapendekezo ya marekebisho ya sheria mbalimbali yenye lengo la kuboresha mifumo ya utoaji huduma, utekelezaji wa majukumu na kutoa mikanganyiko ya kisheria katika utendaji kwenye Taasisi zilizo chini ya Wizara.

Katika Kikao Kazi hicho kilichofanyika kwenye Ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba tarehe 11 Agosti, 2023 na kuhudhuriwa na Menejimenti ya Wizara na kuwashirikisha Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, miswada ishirini na tatu ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria iliwasilishwa na kujadiliwa. Mhe. Ndumbaro pamoja na mambo mengine alisisitiza tafiti za kisayansi kuendelea kufanyika kabla ya mapendekezo yoyote ya mabadiliko ya sheria. 

Mapendekezo ya kurekebisha ya sheria hizo yaliwasilishwa na Bw. Abdulrahman Mshamu Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria kwa Umma.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA