HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA KUWA ENDELEVU.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro akitoa ufafanuzi wa jambo alipokuwa akiongea na  Mkurugenzi Mtendaji wa LSF  Bi Lulu Ng'wanakila  tarehe  03 Agost 2023 Jijini Dar es salaam.   

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na Felix Chakila - WKS Dar es Salaam

Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mtandao wa Watoa Huduma ya Msaada wa Kisheria (TANLAP) na Menejimenti ya Legal Services Facility “LSF” tarehe 03 Agosti, 2023 jijini Dar es Salaam na kujadili masuala ya msaada wa kisheria na ufahamu wa masuala ya sheria ili kuona namna ya kuwa huduma ya msaada wa kisheri inavyokua endelevu nchini.

“Ni vyema mara baada ya kutekeleza Kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Sheria katika mkoa husika kukawa jitihada za kuifanya Kampeni kuwa endelevu ili wanachi waendelee kupata huduma. Niwasihi TANLAP na wadau wengine wakiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika kutumia Ofisi ambazo zipo katika maeneo husika na kuwezesha migogoro iliyoibuka iweze kushughulikiwa.” Alisema Dkt. Ndumbaro.

Katika mazungumzo hayo, Uongozi wa TANLAP umewasilisha ombi kwa Serikali kuendelea kuangalia kwa jicho la ukaribu Sheria zinazohusu ndoa na mirathi kwa kuwa zimekua zikiongezeka kwa kiwango kikubwa na pia ipo haja ya Serikali kuongeza rasilimali watu katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki cha Temeke kinachoshughulikia migogoro ya Mirathi na Ndoa.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA