KAMATI YAPOKEA TAARIFA YA UTENDAJI WA WIZARA NA TAASISI ZAKE
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akitoa ufafanuzi kwenye kikao na ya Kamati ya Kudumu ya bunge Katiba na Sheria wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Wizara kwenye ukumbi wa bunge leo tarehe 22 Agosti 2023.Jijini Dodoma
Na.
George Mwakyembe, Emmanuel Msenga, WKS – Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Utawala na Katiba na Sheria imepokea taarifa ya utendaji wa Wizara na Taasisi zake na kuipongeza Wizara namna inavyosimamia Taasisi zake katika kutekeleza majukumu yake ikisema kuwa taarifa inaonesha Wizara imekuwa na Ushirikiano wa karibu na Taasisi zake ili kuhakikisha utendaji wa kazi unafanyika kwa weledi na kushirikiana.
Akiongea
kwenye kikao cha kupokea taarifa ya miezi miatatu ya utekelezaji wa majukumu ya
Wizara pamoja na Taasisi kwa kipindi cha miezi mitatu zilizo chini ya Wizara
leo tarehe 22 Agosti 2023 Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala, Katiba na Sheria
Mhe. Dkt Joseph Mhagama (MB) amesema naipongeza Wizara kwa jitahada nzuri
zinafanywa kwa kusimamia Taasisi na kujenga shirikiano ambao umekuwa na
mafanikio katika majukumu yenu”
Katika
kikao hicho viongozi wa Taasisi wamefanikiwa kuwasilisha mafanikio yao na
changamoto za Taasisi zao, Taasisi zilizowasilisha taarifa ya utendaji ni Tume
ya Utumishi wa Mahakama, Ofisi ya Serikali ya Mwendesha Mashtaka, Tume ya
Kurekebisha Sheria, pamoja na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA)
ambao wote walielezea mafanikioa na changamoto zinazowakabili wakati wa
utekelezaji wa majukumu. Moja ya changamoto ambayo imekuwa mtambuka kwa taasisi
zote ni upungufu wa rasilimali watu. Akijibu maswali yalioulizwa na wajumbe
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo amesema Wizara pamoja
na Taasisi bado idadi ya watumishi haitoshi na majukumu yamekuwa mengi na
watumishi wamekuwa wakijotoa kufanya kazi hadi muda wa ziada.
Aidha
mjumbe wa Kamati Mhe. Dkt Kaijage amezisisitiza Taasisi hizo kushughulikia
masuala mbalimbali ya wafanyakazi wa Wizara na taasisi hizo, ikiwemo upatikanaji
wa makazi ya wafanyakazi, kupandishwa vyeo wafanyakazi wao wenye sifa, “Kuna
wafanyakazi ambao hawajapandishwa madaraja muda mrefu sana hao muwapandishe ili
kuwapa morali na kazi, alisema Mhe. Kaijage.
Naye Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Pauline Gekul, ameishukuru Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kwa pongezi pamoja na maoni ya kuhusu
taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara na Taasisi hizo, na kuahidi
kuendelea kushirikiana bega kwa bega na taasisi hizo ili kuimarisha utendaji wa
taasisi hizo ambazo zina manufaa kwa wananchi.
“Tukushukuru Ndugu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa kamati hii kwa maoni yenu, sisi kama Wizara pamoja na taasisi zetu zote niwaahidi tutayafanyia kazi maoni haya, na kuongeza ushirikiano baina yetu ili kuboresha utendaji zaidi”
Comments
Post a Comment