MAHAKAMA KUENDELEA NA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA UJENZI WA MAHAKAMA NCHINI – MHE GEKUL


 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akijibu maswali bungeni leo tarehe 30 Agosti 2023 . Dodoma.

Na. George Mwakyembe - WKS DODOMA.      

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul ameeleza kuwa Mahakama inaendelea na mpango wa kujenga ofisi za Mahakama nchini kote na kwamba hadi sasa ofisi 18 za Mahakama za Wilaya zimeshajengwa na Mahakama za Mwanzo ni 71. Mahakama hizi zinajengwa kwa utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024

Mhe. Gekul ameyasema hayo leo tarehe 30 Agosti 2023 bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini Mhe, Daimu Idd Mpakate ambaye aliuliza lini Mahakama itajenga Mahakama za mwanzo katika Tarafa ya Nalasi, Lukumbule, pamoja na Tarafa ya Namasakata.

Pia, Mhe. Gekul amefafanua kuwa tayari Mahakama ya mwanzo ya Nalasi inajengwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa mahakama 71 za mwazo ambazo zitajengwa nchi nzima na tayari mshauri elekezi ameanza kazi na ujenzi utaanza Oktoba 2023. Vilevile, Mhe Gekul ameleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/ 2024 moja ya Mahakama za Wilaya zitakazojengwa ni Mahakama ya Wilaya ya Tunduru.

Aidha, Mhe. Gekul ameleza kuwa Mahakama nchini ina magari mawaili ya (Mobile Court) ambayo yamekuwa yakihudumia Mikoa yenye watu wengi ambayo ni Kagera, Tanga, Arusha, Morogoro, Dar es Salaam.  Mbali ya hizo Mobile Courts kuwa msaada mkubwa katika kupunguza malimbikizo ya kesi, gharama za kuziendesha ni kubwa hivyo mpango wa Serikali ni kujenga Mahakama ili kupunguza gharama za uendeshaji.

Pia Mhe. Gekul alifafanua zaidi namna jinsi Serikali ilivyojipanga kujenga Mahakama za Wilaya 18 na  ambazo  zitajengwa kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024 na miongozi mwa Mahakama hizo ni Mahakama ya Wilaya ya Mbulu ambayo miundombinu yake imechakaa pamoja na Mahakama za Wiliya zingine. Mahakama hizi zinajengwa ikiwa ni utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA