MAKONDO AFANYA ZIARA YA KIKAZI IRINGA


 Bi Mary Makondo ( katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na watalaamu kutoka PPPRA baada  kumaliza mafunzo ya mfumo wa  manunuzi NeST yanayoendelea Mkoani Iringa . Kushoto kwakwe ni Naibu katibu Mkuu  Dkt Khatibu Kazungu . 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi Mary Makondo amefanya ziara ya kikazi mkoani Iringa ambapo katika ziara hiyo amefanikiwa kushiriki mafunzo ya mfumo wa NeST yaliyotolewa na wataalam kutoka PPRA.

Aidha, Katibu Mkuu ametembelea timu ya Wataalam wa PPRA wanaojenga na kutoa huduma za mfumo wa NeST na akawapongeza pia akiwataka waongeze juhudi katika kuhakikisha mfumo unakuwa rafiki na hivyo kuboresha taratibu za manunuzi zitakazowezesha taifa kuboresha huduma za serikali kwa wananchi kwa ujumla.

Katika hatua nyingine akiwa Mkoani Iringa, Bi Makondo ametembelea na Kuzungumza na Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoani Iringa na kujadili mambo mbalimbali yahusuyo utendaji wao wa kazi, Muono Mbele, mafanikio na Changamoto zao.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA