MHE GEKUL AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI MPANGO KAZI WA TAIFA WA HAKI ZA BINADAMU NA BIASHARA
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akihutubia katika kikao cha kujadili Mpango kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu na Biashara, kilicho anadaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa Kushirikiana na Shirika na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), katika ukumbi wa Morena Hotel tarehe 25 Agosti 2023 jijini Dodoma.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience K. Ntwina,
akizungumza wakati wa kikao cha Kujadili mpango Kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu
na Biashara kilichoandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, leo tarehe 25 Agosti
2023, katika ukumbi wa Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na, George Mwakyembe, Emmanuel Msenga, Faraja Mhise - WKS
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (MB) ameongoza kikao cha kujadili mpango kazi wa Taifa wa Haki za Binadamu na Biashara (National Action Plan on Business and Human Right in Tanzania Mainland and Zanzibar) kilicholenga kuangazia masuala ya Haki za Binadamu hasa kwenye nyanja ya biashara kama vile uwekezaji pamoja na shughuli zingine za kibiashara huku ukizingatia masaula ya haki za binadamu wakati wa utekelezaji wake.
Kikao hicho ambacho kimehusisha Wizara na Taasisi mbalimbali kimefanyika tarehe 25 Agosti 2023 katika ukumbi wa Morena Jijini Dodoma.
Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul, ambaye alilkuwa mgeni rasmi ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kushirikiana vyema na Wizara mbalimbali, Idara za Serikali, Taasisi za Umma, Sekta binafsi, Asasi za kiraia, pamoja na wafanyabiashara na wadau wa maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Mhe. Gekul ameongeza kuwa malengo ya Kikao hiki ni moja kati ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kushirikisha wadau mbalimbali katika mchakato wa kuandaa mpango wa kitaifa wa Haki za Binadamu na biashara pamoja uwekezaji.
Aidha , Mhe Gekul ameitaja Tanzania, kuwa ni moja kati ya nchi kumi zilizoanzisha mpango huu, kati ya Nchi hamsini na nne za Afrika.
Wakati huohuo Gekul ameipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kupata hadhi ya daraja ‘A’, ya Mtandao wa Taasisi za Kimataifa za Haki za Binadamu ulimwenguni.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mohamed Khamis Hamad aligusia ukuhimu wa masuala ya haki za binadamu katika uwekezaji ili kuondoa manyanyaso na ukiukwaji haki
“Ni vyema uwekezaji ukazingatia Haki za Binadamu na kuzilinda , tayari nchi za Kenya na Uganda walisha andaa mpango kazi huo na sasa wapo kwenye utekelezaji”.
Akiongea kwenye kikao hicho, Mshauri wa masuala ya utawala bora kutoka shirika la Maendele la umoja wa matafa Bw. Godfrey Mulisa amesema Haki za Binadamu na biashara ni uwanja mpana sana utakaowasaidia wafanyabiashara katika ufanyaji wa biashara zao huku wakizingatia haki za Binadamu.
Pia ameahidi kuwa umoja wa mataifa wataendelea kushirikiana na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika utakelezaji wa mpango kazi huu.
Aidha, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Patience Ntwina ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano wanaowapa katika kutekeleza suala zima la Haki za Binadamu. Pia Bw. Ntwina ameongeza kuwa mchakato wa kuandaa mpango kazi wa Haki za Binadamu na biashara umetokana na andiko ambalo liliwasilishwa katika Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kufanyika vikao kadhaa ambapo walipendekeza kuwepo na majadiliano ambayo yatawahusisha wadau mbalimbali ili kufanikisha mpango kazi huu hivyo leo ni fursa kutoa mapendezo na maoni ili kuweza kuboresha mpango kazi huu kwa maendeleo endelevu ya Taifa.
Kikao hicho ambacho kimeandaliwa na
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora(CHRAGG) kwa kushirikiana na Shirika la
Maenedeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa lengo la kuwajengea uelewa wa
kuzingatia masauala ya Haki za Binadamu wakati wa utekelezaji wa biashara na
uwekezaji.
|
|
Comments
Post a Comment