MHE.GEKUL AWASILISHA SHERIA NDOGO KWENYE KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiwasilisha mapendekezo ya Sheria ndogo ya kumlinda mtoa taarifa na ushahidi (WHISTLEBLOWER AND WITNESS PROTECTION ACT, CAP 446) katika kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, katika ukumbi wa Bunge leo tarehe 24 Agosti 2023 jijini Dodoma.

 

Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, ikifuatilia wasilisho la sheria ndogo lililowasilishwa kwenye Kamati hiyo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul  katika ukumbi wa Bunge leo tarehe 24 Agost 2023 jijini Dodoma.


Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Burton A Mwasomola, akichangia katika wasilisho la Sheria ndogo ya Kumlinda Mtoa taarifa na Mshahidi (WHISTLEBLOWER AND WITNESS PROTECTION ACT, CAP 446), katika Kamati ya kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, katika ukumbi wa Bunge wa  leo tarehe 24 Agosti 2023.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na, George Mwakyembe, Emmanuel Msenga – WKS      

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewasilisha sheria ndogo ya kumlinda mtoa taarifa pamoja na mashahidi (The WhistleBlower and Witness Protection Act Cap. 446), katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo. Akiwasilisha mbele ya kamati Mhe.Gekul ameiambia kamati kuwa sheria hii ni muhimu na itasaidia katika kumlinda mtoa  taarifa pamoja na ushaidi na kumpa mwongozo wa kudai haki zake  mara tu baada ya ushaidi kukamilika.

Mhe, Gekul amewasilisha Sheria hiyo leo tarehe 24, Agosti 2023 Kwenye ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma na kuwataka wajumbe watoe maoni pamoja mapendekezo ili kuweza kuboresha zaidi.

Kikao hicho ambacho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati  ya  Kudumu ya Bunge ya Sheria  ndogo Mhe. Ramadhan Suleiman Ramadhan (MB), ametoa mapendekezo ya kuwa katika sheria hii kuwepo na muundo mmoja wa uandishi wa barua ambao utatumika kujibu barua ya mwombaji wa ulinzi, ilikuepusha utofauti katika kujibu maombi hayo.

Vile vile kamati imependekeza kuwa muda wa Waziri kufanya maamuzi juu ya rufaa ya mwombaji wa ulinzi iwe ni siku 21 tu na si ndani ya siku 30 kama inavyoonyesha sasa. Hivyo kamati imetaka Waziri pamoja na watalaamu kufanya marekebisho katika vifungu hivyo.

 Aidha, Kamati ipendekeza kuwa mwombaji apewe taarifa ya kukubaliwa au kukataliwa  ombi la  kulindwa kwa  ndai ya siku 14 na iwapo mwombaji hataridhika basi anaweza kukata rufaa  kwa Waziri wa Katiba na Sheria. 

Naibu Waziri Gekul ameishukuru Kamati kwa mapendekezo pamoja na maoni waliyotoa na kuahidi kufanyiwa kazi  na kuleta  sheria hiyo ambayo itakuwa imezingatia maboresho  na maoni yote waliyopendekeza. 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA