RAIS SAMIA ACHANGIA UJENZI WA KANISA LA MT. BARNABA - NGUMBO .


 Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Damasi Ndumbaro  akiongea na waumini wa kanisa la Mt. Barnaba  lilipo Wilaya ya Nyasa  mkoani Ruvuma. tarehe 20 Agosti 2023. 




Waumini wa Kanisa la Mt. Barnaba  lilopo  Wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma wakifurai baada ya Waziri wa Katiba NaSheria  Mhe. Damas Ndumbaro kuwasilisha mchango wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  tarehe 20 Agosti 2023. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki katika Ibada ya Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Barnaba-Ngumbo lililopo Kijiji cha Ngumbo,Wilaya ya Nyasa. 

Katiba Ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Mhe. Filberto Sanga, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mhe.Ndumbaro amewaasa wananchi wa Kijiji cha Ngumbo kuendelea kumcha Mungu na kumjengea Mungu nyumba ya Ibada kwa kuwa Mungu mwenyewe katika maandiko matakatifu ameahidi kutuletea amani kupitia nyumba za Ibada huku akiwaasa viongozi kutekeleza majukumu yao ya kiroho na si kutumika kisiasa kunakopelekea kuwachanganya waumini wanaowaongoza.

Katika Ibada hiyo Mhe. Ndumbaro amewasilisha salamu za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuunga mkono juhudi za ujenzi wa Kanisa hilo kwa kuchangia Shilingi Milioni Tano.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA