“TUNABORESHA MIFUMO KWA LENGO LA KUIMARISHA UTENDAJI”- GEKUL


Naibu waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul(MB)akihutubia kwenye hafla ya kuzindu mfumo wa mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mashtaka leo tarehe 23 Agosti 2023 Jijini Dodoma.


Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Simbachawene(MB) akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul(MB) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo wakifuatilia uwasilishwaji wa mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai leo tarehe 23Agosti 2023 Jijini Dodoma. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo akizungumza na Watalaamu kwenye hafla ya kuzinduzi mfumo wa kukusanya, kutunza kumbukumbu za kesi jinai kwenye Ukumbi wa Ofisi za Mashtaka leo tarehe 23Agosti 2023 Jijini Dodoma

Mgeni rasmi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menenjimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe George Simbachawene(MB) akiwa katika picha ya pamoja na meza kuu  na  maafisa kutoka ofisi ya Taifa ya Mashtaka leo tarehe 23Agosti 2023 Jijini Dodoma. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na, George Mwakyembe, Emmanuel Msenga – WKS

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya vitendea kazi kwa watumishi ikiwemo mifumo mbalimbali kwa lengo la kuimarisha na kurahisisha utekelezaji wa majukumu wenye tija kwa watanzania wote kwa ujumla. 

Mhe Gekul ameyasema hayo tarehe 23 Agosti 2023 wakati wa hafla ya makabidhiano ya mfumo wa kielektroniki wa kukusanya, kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi jinai (Case Management Infomation System).

Aidha, Gekul ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa kuanzisha mfumo huu ambao utakua ni kiungo muhimu katika utendaji kazi pia kutoa haki kwa wakati ili kupunguza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wananchi juu ya utendaji wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka, na kusaidia kutoa haki kwa wakati. ‘Haki iliyo cheleweshwa ni sawa na haki iliyovunjwa’ alisema Mhe. Gekul.  

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala na Bora Mhe. George Simbachawene, ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema “Tunatambua umuhimu wa mfumo huu kwani unaendana na maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anasisitiza utekelezaji kujikita kwenye jukwaa la kidijitali na kuhakikisha mifumo hiyo inasomana” 

Mhe. Simbachawene ameongeza kuwa mfumo huu utasaidia kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Mashtaka katika kushughulika kesi mbalimbali, ambapo kwa ujumla utaweka wazi na kupunguza malalamiko kwa wananchi juu ya maamuzi ya mahakama yanayotolewa. “Ni kama tulikua gizani, kwa dunia ya leo unapokuwa hauna mifumo mizuri, dunia ya sasa kila jambo linafanyika kwa kutumia mifumo  ili kusaidia kuraisisha utendaji kazi, kwa hiyo hongereni sana kwa hatua hii”. Alisema Mhe. Simbachawene.

Naye Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Marry Makondo amesema “Leo tunashuhudia maboresho uwekezaji wa mifumo ambayo inaleta ufanisi katika utendaji kazi na kuokoa rasilimali muda, na kuhakikisha wananchi wanapatiwa haki kwa wakati”. 

Aidha, Bi. Makondo ameishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao (E-GA pamoja na wadau wote kwa kufanikisha utengenezaji wa mfumo huo.

Mfumo huo ambao umetengezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa Mashtaka ili kuimarisha utendaji kazi pamoja na kutunza kumbukumbu za kesi jinai nchini.

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA