WANANCHI WAJITOKEZA KUPATA ELIMU YA SHERIA KWENYE MAONESHO YA NANENANE

 Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Lilian Kilembe akiwasikiliza wananchi waliotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria Katika Maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jjijini Mbeya.

Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Lilian Kilembe akiwaimbisha wananfunzi wa shule ya seokondari  Uwindi  wimbo wa “DON’T TOUCH”   baada ya kutembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria Katika Maonyesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jjijini Mbeya.


Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Uwindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa kitengo cha Uangalizi wa Utajili wa asili na Mali asilia za nchi Bi. Neema Mwanga walipotembelea banda la Wizara ya Katiba na Sheria  katika maonesho ya nane nane yanaoyendelea katika viwanja ya John Mwakangale Jijini Mbeya                

XXXXXXXXXXXXXXX

      Na. George Mwakyembe - WKS Mbeya. 

Banda la Wizara ya Katiba na Sheria ililopo katika viwanja vya maonesho ya Nanenane katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ambapo maonesho haya kwa mwaka huu yanafanyika kitaifa na kimataifa mkoani humo limeendelea kupokea wateja kwa wingi wanaofika kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Miongoni mwa wateja wanaotembelea banda hilo ni wanafunzi ambao walitaka kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu elimu ya ukatili wa kijinsia na nini wanachotakiwa kufanya mara mtu anapopatwa na janga hilo. Pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika kwa wingi kupata elimu ya sheria pamoja na msaada wa kisheria. Kundi kubwa la wananchi wamekuwa wakiuliza maswali yanayohusu kuhusu uandikaji wa wosia, haki za binadamu pamoja na kupata msaada wa kisheria wa namna ya kutatua migogoro ya ardhi, miradhi pamoja na ndoa.  

Maoneosho ya Nane nane yanafanyika kwa mara ya kwanza kimataifa jijini hapa lakini ikiwa ni ya tisa kufanyika mkoani Mbeya kitaifa yakiongozwa na kauli mbiu “Vijana na Wanawake ni Msingi imara wa mifumo ya Chakula”. Maonesho haya yatafikia tamati Agosti 8 huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA