
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kwenye picha ya pamoja baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan (kulia) alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea alipokutana na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan. 27/09/2023 Jijini Dar es Salaam. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na Balozi wa Urusi nchini Mhe. Andrey Avetisyan na kufanya majadiliano ya namna bora ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali hasa katika Sekta ya Sheria. Kikao hicho kimefanyikia tarehe 27/09/2023 katika Ukumbi wa Ofisi za Wakala wa Usajili, Udhamini na Ufilisi (RITA) Jijini Dar es Salaam ambapo moja ya eneo lililogusiwa katika mazungumzo hayo ni kuimarisha mifumo ya Haki ambapo Balozi Aveti...