MAAFISA WA USTAWI WA JAMII NI WADAU MUHIMU WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA – GEKUL
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akioongea na Maafisa Ustawi wa jamii hawapo pichani kwenye kikao kilichoandaliwa na Wizara ya Maendele ya Jamii tarehe 06 September Jijini Dodoma.
Na Lusajo Mwakabuku & Candid Nasua –
WKS Dodoma
Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amesema Wizara kupitia Taasisi zake
zikiwemo Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya
Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu kwa pamoja zimekuwa zikifanya
kazi kwa ukaribu na Maafisa wa Ustawi wa Jamii katika utekelezaji wa majukumu
yao.
Mhe. Naibu
Waziri ameyasema hayo wakati akimwakilisha Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.
Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Ustawi
wa Jamii ulioandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum, tarehe 06 Septemba, 2023 Jijini Dodoma.
Akitoa
salaam za Wizara katika mkutano huo, Mhe. Gekul alielezea namna ambavyo Wizara
imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Maendeleo ya Jamii hususan katika
utekelezaji wa Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria za Ndoa mwaka 1971, Sheria ya
Mtoto mwaka 2009 na Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.
Pamoja na
hayo, aliongeza kuwa, Wizara kupitia wataalam iliwasilisha maoni yao wakati wa
mchakato wa upatikanaji wa Mwongozo wa Taifa wa uendeshaji, usimamizi na
uratibu wa Mabaraza ya usuluhishi wa migogoro ya ndoa mwaka 2023 ambao leo hii
ni moja ya Miongozo iliyokuwa inazinduliwa wakati wa Mkutano huu.
Mhe. Gekul
aliongeza kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ni mdau mkubwa wa masuala ya Ustawi
wa Jamii, na kwamba Wizara inaunga mkono jitihada zote zinazochukuliwa na
Serikali kuhusu masuala ya ustawi wa jamii ikiwepo kusimamia Sheria mbalimbali
ikiwemo mchakato wa kukamilisha maboresho ya Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971,
ambao upo mbioni kukamilika na kwamba Wizara ina imani kabisa mchakato wa
mabadiliko utakamilika hali itakayomsaidia kumwepusha mtoto wa kike na madhila
yakuolewa katika umri mdogo.
Katika
mkutano huo Mhe. Naibu Waziri alimwakilisha Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria
naye Mhe. Dkt. Dotto Biteko Naibu Waziri Mkuu alimwakilisha Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philipo Isdor Mpango.
Comments
Post a Comment