“UKIKIUKA UTII WA SHERIA UTAENDELEA KUWA MTEJA WETU” WAZIRI CHANA.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023. 


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akiongea na watumishi wa ofisi ya Taifa ya Mashtaka Mkoa wa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023.

Watumishi wa ofisi Taifa ya Mashtaka mkoa wa Iringa wakimsikiza waziri wa katiba na sheria Mhe. Balozi Pindi Chana alipofanya ziara katika ofisi hizo mkoani Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika  picha ya pamoja watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa Iringa leo tarehe 25 Septemba 2023. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXX 

Na, George Mwakyembe – WKS Iringa. 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana amekemea vikali vitendo vyote vya ukatili unaofanywa na baadhi ya watu katika jamii zetu na kuwakumbusha kuwa vyombo vya haki anavyovisimamia vipo imara na makini katika kuhakikisha kila mtanzania anaishi kwa amani na hivyo kuitunza tunu yetu ya amani tuliyojijengea kwa muda mrefu.

Waziri Chana ameyasema hayo leo tarehe 25 Septemba 2023 alipokuwa akipokea taarifa ya utendaji kazi kwa Ofisi ya Mashtaka Mkoa wa Iringa pamoja na taarifa ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Iringa ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembele ofisi za taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.

Akitoa taarifa kwa Waziri Chana juu ya utendaji kazi ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Iringa Bw. Basilius Namkambe alisema kumekuwa na ongezeko la vitendo vya ukatili katika Mkoa wa Iringa hasa wakati wa mavuno ya pombe aina ya ulanzi.

“Vitendo hivi vimekuwa vikifanyika na hatua zimekuwa zikichukuliwa, changamoto katika hili imekuwa ni kutojitokeza katika kutoa ushahidi mahakamani wakati wa kuendesha kesi, na hii imekuwa changamoto kubwa sana kwa mkoa wetu wa Iringa na tayari kwa mwaka huu tuna kesi  za makosa ya kubaka 129  kati ya hizo 83  zimeshia Mahakamani na  na kesi 46 bado zinaendelea” Alisema Bw. Namkambe.

Akiongea baada ya kupokea taarifa hizo Mhe. Chana amewasiii watendaji hao kutokata tamaa ya kuwachulia hatua kali wale wote wanafanya vitendo vya ukali na pia wale wanaokiuka sheria za nchi yetu, “nchi hii ina amani na utulivu, anayejichulia sheria mkononi basi achukuliwe hatua kali za kisheria” Alisema Mhe, Chana.

Pia Mhe. Chana alipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa Mkoa wa Iringa huku akiwapongeza watendaji hao kwa kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 6 kutoka katika mashauri 28 yaliyokuwa yakiendelea mahakamani kwa kipindi cha nusu mwaka yaani kutoka Januari mpaka Septemba 2023.

“Nawapongeza sana kwa kazi kubwa mliyofanya ya kuitetea pamoja na kuiwakilisha Serikali katika mashauri mbalimbali yaliyopo Mahakamani na hatimaye kuokoa kiasi cha shilingi bilioni 6, hizi ni juhudi kubwa sana na fedha hizi zitatumika katika  miradi  ya maendeleo ya watanzania” Alisema Mhe, Chana.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu na Usimamizi wa Kesi ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Bw. Camilius Ruhinda amemshukuru Mhe. Chana kwa kufanya ziara katika ofisi hizo na kumwahidi kuendelea kutoa ushirikiano na Wizara katika mashauriano mbalimbali. 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA