WAZIRI CHANA AIPONGEZA TUME YA KUREKEBISHA SHERIA


 

Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma.


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana akiongea na watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria katika ofisi zao zilizopo udom leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma.   

Watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana katika ofisi zao zilizopo UDOM leo tarehe 22 Septemba 2023 Jijini Dodoma. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na George Mwakyembe & Faraja Mhise - WKS.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na menejimenti pamoja watumishi wa Tume ya Kurekebisha Sheria ikiwa ni muendelezo wa ziara zake zenye lengo la kuyafahamu majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria tangu ateuliwe kuwa Waziri wa Wizara hii.  

Akiongea na watumishi hao leo tarehe 22 Septemba, 2023 katika ofisi za Tume ya Kurekebisha Sheria zilizopo Jijini Dodoma, Mhe. Chana amewapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ya utafiti wa marekebisho ya Sheria pamoja na kutunga Sheria mpya zenye kuendana na wakati. 

 “Tume hii imekuwa ikifanya vizuri katika ukanda wa Afrika mashariki pamoja na ukanda wa Kusini mwa bara la Afrika na imekuwa mfano wa kuigwa, pia Tume hii imekuwa ikifanya mapitio mbalimbali ya Sheria muhimu katika nchi yetu, na  wanasheria kutoka nchi nyingine  wamekuwa wakija kujifunza hapa nawapongeza sana “ amesema Mhe. Chana. 

Aidha, Mhe. Chana ameongeza kuwa Tanzania ni nchi yenye amani, utulivu pamoja na usalama   kwasababu ya kuzingatia Sheria na taratibu za misingi bora ambayo imewekwa. Waziri Chana aliongeza kuwa Sheria za Tanzania ni bora na ubora wake unatokana na utafiti mzuri unaofanyika kabla ya kuzitunga sheria hizo lakini pia marekebisho ya Sheria zenyewe yanayofanyika kila inapohitajika. 

Pamoja na pongezi hizo pia Mhe. Chana alipokea ripoti za mapitio ya mfumo wa sheria inayohusu mdhamini na mapitio ya mfumo wa Sheria inayohusu maadili ambayo imefanyiwa utafiti na Tume ya kurekebisha Sheria. Mhe, Chana amehaidi kushirikiana na Tume katika kushughurikia mambo kadhaa ya kiutendaji yanayoikabili Tume ikiwemo upungufu wa watumishi ili kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo yaTume na Wizara. 

Katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu alisema ufanyaji wa tafiti za Sheria ambazo zinakidhi mahitaji kutokana na wakati  uliopo ni mkakati wa Wizara katika kuhakikisha Sheria ambazo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho basi zinafanyiwa tafaiti ili ziweze kurekebishwa.   

Naye, Mwenyekiti wa Tume Jaji mstaafu January Msofe amempongeza Waziri Chana kwa kuendelea kuaminiwa na Mhe, Rais na kuteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Mwenyekiti wa huyo akagusia baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Tume ya Haki ya Jinai likiwemo suala la maadili, vifungo vya watoto, ulipaji wa fidia  kwa wathirika na vifungo, kuwa yote hayo  yanafanyiwa utafiti  ili kupata Sheria zilizo bora na tayari wamejipanga kuhakikisha kuwa  yote yaliyopendekezwa  na Tume ya Haki jinai yanafanyiwa kazi  kwa manufaa ya watanzania. 

 

 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA