Posts

Showing posts from October, 2023

DKT. CHANA AZINDUA KITABU “THE FATIMIDS”

Image
  Wazi ri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia kabla ya kuzindua kitabu ‘’THE FATIMIDS’’ tarehe 25 Oktoba, 2023 Jijini Dar es Salaam. Wazi ri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (kulia) na mwandishi wa kitabu Dkt. Shainool Jiwa baada ya uzinduzi wa kitabu ‘’THE FATIMIDS’’ tarehe 25 Oktoba, 2023 Jijini Dar es Salaam. Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana wakati wa hafla ya kuzindua kitabu ‘’THE FATIMIDS’’ tarehe 25 Oktoba, 2023 Jijini Dar es Salaam. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Wazi ri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amezindua Kitabu cha Historia ya Utawala wa Kiislamu wa Fatimid ‘’THE FATIMIDS’’ huku akimpongeza mwandishi wa kitabu hicho mwanamama Dkt. Shainool Jiwa kutoka Taasisi ya Aga Khan na kuwahimiza mabinti walioko mashuleni na vyuoni kuiga mfano. Kitabu hicho kinachoelezea utawala wa Kiislamu unaosemekana kutawala zaidi ya miaka 250 katika mwambao wa bahari ya Atlantik...

KAMATI YA BUNGE YAPOKEA UFAFANUZI WA SERIKALI KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA

Image
Naibu Waziri wa  Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  tarehe 23 Oktoba ,2023. Ofisi za Bunge Dododma.  XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX N a, William Mabusi - WKS Dodoma. Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imepokea ufafanuzi wa Serikali wa baadhi ya vifungu vya sheria katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria namba 3 wa mwaka 2023 na Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2023 yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria mbalimbali nchini. Ufafanuzi huo wa Serikali umetolewa na Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.  Jaji  Dkt. Eliezer Feleshi na Wataalam wa Wizara kwa kujibu hoja za Wabunge tarehe 23 Oktoba, 2023 kwenye kikao kati ya  Kamati na Wizara pamoja na Taasisi zake kilichofanyika ofisi za Bunge, Dodoma. Katika k...

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUWEKA MIFUMO SHIRIKISHI KATIKA KUIMARISHA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Image
  Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe, Mathew Mwaimu( Jaji Mstaafu ) akizungumza  kwenye kikao cha 77 cha Tume ya Haki za binadamu na watu Oktoba 23,2023 Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na. Lusajo Mwakabuku- WKS Arusha Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutengeneza mifumo shirikishi yenye lengo la kukuza na kuimarisha haki za binadamu na watu nchini. Mhe. Jaji Mwaimu ametoa pongezi hizo tarehe 23 Oktoba 2023 wakati akihutubia wajumbe wa Kikao cha Kawaida cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachoendelea jijini Arusha. Mhe. Jaji Mwaimu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa kuweka mifumo shirikishi inayowezesha wadau mbalimbali kujadili mambo muhimu ya kitaifa ikiwemo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ikiwa ni jitihada za Seri...

RAIS DKT. SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA NA TUME YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU

Image
  Waziri wa Katiba na  Sheria  Mhe. Balozi Pindi Chana (Mb)akitoa neno la shukran mara baada ya kupokea Tunzo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania  Mhe.Dkt Samia suluhu Hassan  katika Kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu  na Watu Oktoba 21,2023 Arusha. Waziri wa Katiba  na Sheria  Mhe.Balozi  Pindi Chana(Mb)akipokea Tunzo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri  ya Muungano  wa Tanzania  Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kutoka kwa Viongozi  wa Tume ya Afrika  ya Haki za Binadamu na Watu Oktoba 21,2023 Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na Lusajo Mwakabuku & Rosemary Mlale - Arusha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu imemtunukia Tuzo ya Heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake katika kutetea, kulinda na kuimarisha haki za binadamu katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri wa ...

NAIBU WAZIRI GEKUL APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA CHUO CHA IJA

Image
  Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akipitia ripoti ya Utekelezaji wa shughuli za Chuo cha Mahakama Lushoto wakati ikiwasilishwa na Naibu Mkuu wa chuo Dkt. Goodluck Chuwa, tarehe 18 Oktoba, 2023 Jijini Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na George Mwakyembe – WKS Dodoma. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za chuo cha Mahakama Lushoto na kuwaasa kufungua matawi ya chuo maeneo mengine nchini kama vile Dodoma na baadhi ya maeneo mengine. Mhe. Gekul amepokea taarifa hiyo tarehe 18 Oktoba, 2023 Jijini Dodoma na kuwaasa kuwa ni vyema sasa chuo cha Mahakama Lushoto kikawa na matawi katika mikoa mbalimbali ili kuruhusu watoto wengi wa kitanzania kusoma chuo hicho. Aidha, Gekul amefafanua kuwa mbali ya kutoa mafunzo ya Majaji lakini pia chuo hicho kijikite katika kutoa mafunzo katika kada nyingine za sheria kama vile mafunzo kwa Makatibu wa Majaji na pia mafunzo kwa wanasheria. Naye Naibu Mkuu wa ch...

WAZIRI CHANA AWASILISHA MSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA KWENYE KAMATI YA BUNGE

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Sheria Baada ya kuwasilisha Mswada wa Marekebisho ya Sheria.tarehe 18 Oktoba 2023 Ukumbi wa Bunge Dodoma. Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala , Katiba na Sheria kilichotokaa kupokea wasilisho la Mswada  wa Marekebishoi ya Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, tarehe 18 Oktoba 2023 Ukumbi wa Bunge Dododma.   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe & William Mabusi - WKS Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amewasilisha Mswada wa marekebisho ya sheria 23 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria yaliyolenga kuondoa upungufu uliobainika wakati wa utekelezaji wa sheria hizo. Mhe. Chana amewasilisha mapendekezo ya marekebisho hayo tarehe 18 Oktoba, 2023 kwenye ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma. Mhe. Chana amezitaja baadhi ya sheria hizo kuwa ni Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu ...

MHE. CHANA AKUTANA NA KAMATI YA HOUSEHOLD COMMITTEE KUTOKA BUNGE LA AFRIKA KUSINI

Image
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi ChANA akiwa amejifunga zawadi ya vazi alilopewa na wajumbe wa Kamati ya HouseHold Committee on Petitions kutoka Jimbo la  FreeState Bunge la Afrika Kusini  tarehe 18 Oktoba 2023. Jijini Dododma.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi  Dkt Pindi Chana akimkabidhi  zawadi Mwenyekiti  wa Kamati ya House hold Committee on Petitions Kutoka jimbo la Free State Bunge la Afrika kusini  Mhe. William Shabalala  tarehe 18 Oktoba 2023 jijini Dodoma.  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana alipokutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa kamati ya House hold Committee on Petions kutoka Jimbo la Free State Bunge la Afrika Kusini  tarehe 18 Oktoba , 2023  ukumbi wa Bunge Dodoma.   XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Na George Mwakyembe & William Mabusi - WKS Dododma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na wajumbe wa Kamati ya  Househol...

Tukitekeleza Kazi kwa Kasi Hii Tutaelewana: Dkt. Chana

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana wakati akipokea taarifa ya utekelezaji wa Robo Mwaka na Muswada wa marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya sheria, tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul wakati wakipokea taarifa ya utekelezaji wa Robo Mwaka na Muswada wa marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya sheria, tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma. Sehemu ya Viongozi wa taasisi walishiriki kikao kazi cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Robo Mwaka na Muswada wa marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya sheria, tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Dodoma Waziri wa Katiba na Sheria Mhe....

Pelekeni kwa Wananchi Elimu ya Sheria Mliyopata: Dkt. Kazungu

Image
  Bw. Burton Mwasomola Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria akihutubia kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Dkt. Khatibu Kazungu wakati wa kufunga mafunzo ya Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2023, tarehe 13 Oktoba, 2023 Morogoro. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Morogoro Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu ametoa rai kwa washiriki wa mafunzo ya Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2023 kupeleka elimu waliyoipata kwa wananchi ili watambue jitihada zinazofanywa na Serikali za kuendelea kupambana na uhalifu nchini. Dkt. Kazungu ametoa rai kwenye hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Bw. Burton Mwasomola Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba wakati wa kufunga mafunzo ya Sheria ya Ulinzi wa Watoa Taarifa na Mashahidi ya mwaka 2015 na Kanuni zake za mwaka 2023 kwa Maafisa Waandamizi Wachunguzi kutoka Taasisi Chunguz...

Makondo: Tushirikiane Kutunza Amani

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo akihutubia wakati akifungua mafunzo kwa Maafisa Uchunguzi Waandamizi kutoka Taasisi zinazotekeleza Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 12 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ufuatiliaji Haki Bi. Beatrice Mpembo kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, akitoa maelezo ya awali ya mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 12 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo kwenye picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 12 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na William Mabusi – WKS Morogoro Katibu Mkuu wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo ameitaka jamii kuwa mstari wa mbele katika kufichua uhalifu kwa lengo la kuendeleza amani na usalama kwa maslahi mapana ya taifa. Bi. Makondo ameyasema hayo wakati akifungua maf...

Chana Asema Serikali Inathamini Uhai wa Kila Mtu

Image
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akihutubia alipofungua Kongamano kwa ajili ya mjadala kuhusu adhabu ya kifo Tanzania, tarehe 10 Oktoba, 2023 Jijini Dar es Salaam. Sehemu ya Washiriki kwenye Kongamano lililofanyika  Jijini Dar es Salaam kujadili adhabu ya kifo nchini Tanzania, tarehe 10 Oktoba, 2023. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx Na Lusajo Mwakabuku – WKS Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema adhabu ya kifo kwa nchi yetu imekuwa ya lazima pale tu inapohusisha kuondoa uhai wa binadamu mwingine kwani hata katika kosa la uhaini pamoja na kuwa inatoa adhabu ya kifo, bado inatoa nafasi kwa Jaji kuamua vinginevyo isipokuwa pale ambapo kutakuwa kumetokea mauaji ndio adhabu hiyo itakuwa lazima. Waziri Chana ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maadhimisho ya Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani yaliyoandaliwa na TLS leo tarehe 10 Oktoba, 2023 Jijini Dar es salaam. Waziri Chana akaongeza kuwa katika utekelezaji wa she...

Wizara yatoa Mafunzo ya Sheria kwa Waandishi wa Habari

Image
  Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Morogoro, Bi. Neema Haule akihutubia wakati akifungua mafunzo kwa Waandishi wa Habari Waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 10 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Mkurugenzi Msaidizi wa Katiba kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bw. Burton Mwasomola akitoa maelezo ya awali ya mafunzo kwa Waandishi wa Habari Waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 10 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Amani Manyaga akiwasilisha Mada kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 10 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Mwandishi kutoka Fullshangwe blog Bw. John Bukuku akichangia kwenye majadiliano wakati wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Waandamizi kuhusu Sheria na Kanuni za Ulinzi kwa Watoa Taarifa na Mashahidi, tarehe 10 Oktoba, 2023 Mkoani Morogoro. Sehemu ya Washiriki wa mafunzo kwa Waandishi wa Habari Waandamizi kuh...