Chana Asema Serikali Inathamini Uhai wa Kila Mtu
Na Lusajo Mwakabuku – WKS
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema adhabu ya kifo kwa
nchi yetu imekuwa ya lazima pale tu inapohusisha kuondoa uhai wa binadamu
mwingine kwani hata katika kosa la uhaini pamoja na kuwa inatoa adhabu ya kifo,
bado inatoa nafasi kwa Jaji kuamua vinginevyo isipokuwa pale ambapo kutakuwa
kumetokea mauaji ndio adhabu hiyo itakuwa lazima.
Waziri
Chana ameyasema hayo alipokuwa akihutubia katika hafla ya Maadhimisho ya
Kimataifa ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani yaliyoandaliwa na TLS leo tarehe 10
Oktoba, 2023 Jijini Dar es salaam.
Waziri
Chana akaongeza kuwa katika utekelezaji wa sheria nchini mwetu, Tanzania kama
Taifa inathamini haki ya kuishi na imejipambanua kulinda haki hiyo na ndiyo
maana imeweka katika Katiba yake Ibara ya 12 kuwa kuna haki ya kuishi na
inatambua itifaki na mikataba mingi ya kimataifa inayoongelea haki ya kuishi.
Aidha,
Waziri Chana akaongeza kuwa pamoja na kuwa adhabu ya kifo ipo kwa mujibu wa
Sheria, Lakini Serikali bado inathamini
na kulinda uhai wa kila mtanzania na ndiyo maana hata wale waliopewa adhabu ya
kifo wakiumwa wanatibiwa kwa gharama ya Serikali.
Comments
Post a Comment