KAMATI YA BUNGE YAPOKEA UFAFANUZI WA SERIKALI KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul (Mb) akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tarehe 23 Oktoba ,2023. Ofisi za Bunge Dododma.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na, William Mabusi - WKS Dodoma.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,
Katiba na Sheria imepokea ufafanuzi wa Serikali wa baadhi ya vifungu vya sheria
katika Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali za Sekta ya Sheria namba 3 wa
mwaka 2023 na Mswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 4 ya mwaka 2023
yenye lengo la kuboresha utekelezaji wa sheria mbalimbali nchini.
Ufafanuzi
huo wa Serikali umetolewa na Mhe. Pauline Gekul Naibu Waziri wa Katiba na
Sheria kwa kushirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer
Feleshi na Wataalam wa Wizara kwa kujibu hoja za Wabunge tarehe 23 Oktoba, 2023
kwenye kikao kati ya Kamati na Wizara pamoja na Taasisi zake
kilichofanyika ofisi za Bunge, Dodoma.
Katika kikao
hicho, Kamati ilikuwa inasikiliza majibu ya Serikali kupitia majedwali ya ya
Kamati, ambapo Kamati imepokea majibu ya Serikali na kuridhika kupitisha
miswada hiyo yenye jumla ya sheria 33 zinazolenga kubadilishwa.
Awali
akichangia katika kikao hicho Mjumbe wa Kamati Mhe. Abdullah Ali Mwinyi amesifu
mabadiliko hayo kwani yamezingatia mambo mengi akitaja blue print kama mfano,
jambo ambalo litafanya sheria zitakazobadilishwa kuishi muda mrefu kabla ya
kuhitajika mabadiliko mengine.
Akitoa
shukrani kwa Kamati Mhe. Gekul amefurahishwa na uamuzi wa Kamati kuridhia
marekebisho hayo ambayo msingi wake ni kuboresha utendaji wa Serikali.
“Ulimwengu unapobadilika mambo mengi yanajitokeza na hivyo kama nchi ni lazima
kukabiliana na mabadiliko hayo, namna mojawapo ya kukabiliana na mabadiloko
hayo ni mabadiliko ya sheria,” alisema.
Katika hatua
nyingine Kamati hiyo imepokea taarifa ya utekelezaji kutoka Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo
cha Uongozi wa Mahakama Lushoto.
Akichangia
katika taarifa hizo Mhe. Mashimba Ndaki amesema umehimu wa Tume ya Hki za
Binadamu na Utawala Bora unaongezeka kutokana na kuongezedka kwa idadi ya
Watanzaniawa na kuongezeka kwa matukio ya uvunjanji wa haki za binadamu.
Akashauri Tume kuwa na ofisi za Mikoa na Wilaya kuiwezesha kuwa karibu zaidi na
wananchi katika kusimamia haki na utawala bora kwani makundi kama Sungu sungu na
Walizi binafsi wakati mwingine hujichukulia hatua za kusimamia ulinzi huku
wakikiuka haki za binadamu.
Akiahirisha
kikao hicho Kaimu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Florent Kyombo amesema Kamati yake
kwa niaba ya Bunge itaendalea kushirikiana na Wizara na Taasisi zake katika
kuimarisha utendaji wa Wizara ili kuisaidia Serikali kutimiza majukumu yake.
Comments
Post a Comment