Maandalizi ya Kikao Cha 77 Cha Tume ya Haki za Binadamu na Watu Yaiva.
Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Bwana Missaile Musa akitoa neno la ufunguzi na ukaribisho katika kikao cha Makatibu Wakuu na Viongozi wa Taasisi pamoja na Wanakamati ya maandalizi ya kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, kinachotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 9 Novemba mwaka huu. 06/10/2023 Arusha.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi.
Mary Makondo akifurahia jambo na mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Bw. Reuben
Shesha wakati wa kikao cha maandalizi ya kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya
Haki za Binadamu na Watu kinachotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe
20 Oktoba mpaka tarehe 9 Novemba mwaka huu. 06/10/2023 Arusha.
Sehemu ya wanakamati na wajumbe wa maandalizi
ya kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu kinachotarajiwa
kufanyika Jijini Arusha katika kumbi za AICC kuanzia tarehe 20 Oktoba mpaka
tarehe 9 Novemba mwaka huu. 06/10/2023 Arusha.
Picha ya pamoja ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara
zilizoalikwa na Viongozi wengine wa Taasisi mbalimbali za Serikali
kwenye kikao cha maandalizi ya kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za
Binadamu na Watu kinachotarajiwa kufanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 20
Oktoba mpaka tarehe 9 Novemba mwaka huu. 06/10/2023 Arusha.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na. Lusajo Mwakabu – WKS Arusha
Wizara
ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wizara pamoja na Taasisi mbalimbali za Serikali
inaendelea na maandalizi ya kikao cha 77 cha Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu
na Watu kinachotarajiwa kufanyika Jijini Arusha katika kumbi za AICC kuanzia
tarehe 20 Oktoba mpaka tarehe 9 Novemba mwaka huu.
Akielezea
hatua ya maandalizi ya Kikao hicho mbele ya Makatibu Wakuu kutoka Wizara
zilizoalikwa na viongozi wengine wa Taasisi tarehe 06 Oktoba, 2023, Katibu Mkuu
wa Katiba na Sheria Bi. Mary Makondo alisema hatua za maandalizi ya kikao hicho
kinachotarajiwa kuwa na watu wasiopungua 700 yanaendelea vyema hasa kutokana na
ushirikiano unaotolewa Wizara mbalimbali ikiwemo Wizara ya Fedha iliyopitisha
fedha kwa ajili ya kikao hicho.
Aidha,
Katibu Mkuu aliwaomba viongozi na watumishi waliohudhuria kikao hicho cha
maandalizi kupitia taarifa ya kamati ya maandalizi kuiboresha ili iweze
kuwasilishwa kwenye kikao cha Mawaziri na hatimaye kwa pamoja taifa liweze
kufakinisha kikao hicho na kuleta tija kwa watanzania na waafrika kwa ujumla
wake.
“Wizara
ya Katiba na Sheria kama Wizara yenye kuratibu na kusimamia masuala ya Haki za
Binadamu na Watu nchini, inaendelea na maandalizi ya Kikao cha 77 cha Kamisheni
ya Haki za Binadamu na Watu kama ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alivyoelekeza. Mkutano huu unahusisha sekta mbalimbali zaidi ya
masuala ya haki za binadamu na watu, yakiwemo masuala ya ushirikiano wa
kimataifa; utamaduni, sanaa na michezo, fedha na uchumi, ulinzi na usalama,
afya na habari na mawasiliano. Hivyo, niliona upo umuhimu mkubwa wa
kuwashirikisha ninyi kama mamlaka za kimkakati kwenye suala hili muhimu
lililobeba taswira ya kitaifa ili tuweze kujadili na kushauriana kuhusu namna
bora ya kulifanikisha kwa pamoja.” Alisema Bi. Makondo.
Akiielezea
tume hiyo kabla ya kuelezea hatua ya maandalizi ilipofikia, Mkurugenzi wa Haki
za Binadamu kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Nkasori Sarakikya alisema pamoja
na kutekeleza majukumu mengine ambayo Kamisheni hii inaweza kukabidhiwa na
Bunge la Wakuu wa Nchi na Serikali, tume hii pia inatekeleza majukumu makuu
matatu ambayo ni ulinzi wa haki za binadamu na watu, kukuza haki za binadamu na
watu na kutoa tafsiri ya Mkataba wa
Afrika wa Haki za Binadamu na Watu.
Akiongelea
hatua iliyofikiwa, katika ziara hiyo, Mkurugenzi huyo alisema timu ya wataalam
kutoka Kamisheni walikagua na kuchagua ukumbi na ofisi ambazo wanatarajia
kutumia kwenye kikao cha 77 cha Kamisheni ya Haki za Binadamu na Watu. Pia,
walikagua mifumo ya TEHAMA, hoteli na sehemu mbalimbali za malazi kama “self
contained apartments”. Vilevile, pande zote zilifanya majadiliano juu ya
Makubaliano kati ya Serikali na Kamisheni juu ya wajibu wa Serikali kama nchi
mwenyeji wa Kikao cha 77 cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Makatibu Wakuu na wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali walipokea taarifa, wakahoji baadhi ya mambo yaliyotajwa katika taarifa na pia wakajadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika utekelezaji wa maandalizi katika kuhakikisha ukwamuzi kwa mambo yaliyokwama unapatikana na kushauri namna bora katika kuhakikisha mkutano huu unakiwa wa mafanikio.
Tarehe
31 Januari, 2023 Mwenyekiti wa Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu,
Mhe. Kamishna Remy Ngoy Lumbu (kutoka DRC Kongo) alimtembelea Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika mazungumzo na
Mheshimiwa Rais, Mwenyekiti aliwasilisha ombi la Serikali ya Tanzania kuwa
mwenyeji wa kikao cha 77 cha Kawaida cha Kamisheni ya Afrika ya Haki za
Binadamu na Watu huku akimwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awe
Mgeni Rasmi katika mkutano huo. Mhe. Rais aliyakubali maombi yote mawili, na
akaelekeza kwamba kikao hicho kifanyike nchini Tanzania kuanzia Oktoba, 2023
ili mahitaji yake yaweze kufanyiwa kazi wakati wa kuandaa bajeti ya mwaka wa
fedha 2023/24.
Ridhaa
ya mwitikio chanya wa Serikali ya Tanzania iliwasilishwa rasmi kwenye Kamisheni
ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu pamoja na Umoja wa Afrika (AU) wakati wa
mkutano wa Wakuu wa Nchi mwezi Februari, 2023. Kufuatia ridhaa iliyotolewa,
Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliwasilisha maombi yake rasmi
kwa Serikali kuandaa kikao tajwa kuanzia tarehe 20 Oktoba hadi 9 Novemba, 2023.
Comments
Post a Comment