MHE. CHANA AKUTANA NA KAMATI YA HOUSEHOLD COMMITTEE KUTOKA BUNGE LA AFRIKA KUSINI
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na George
Mwakyembe & William Mabusi - WKS Dododma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekutana na
wajumbe wa Kamati ya Household Committee on Petitions kutoka
Jimbo la Free State Bunge la Afrika Kusini na kufanya nao
mazungumzo yanayohusu ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini.
Mhe. Chana amekutana na ujumbe huo tarehe 18 Oktoba, 2023 katika ukumbi
wa Bunge Jijini Dodoma. Katika maongezi hayo Mhe. Chana amesema “Ushirikiano wa
Tanzania na Afrika Kusini ni wa kihistoria na wakipee kwani nchi hizi mbili
zimekuwa zikishirikiana tangu enzi za kupigania uhuru”.
Aidha, Mhe. Chana ameongeza kuwa “hata sasa ushirikiano baina yetu
umeimarika zaidi kwani siyo muda mrefu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan alifanya ziara nchini Afrika Kusini na hii
inadhirisha ni namna gani mahusiano yetu yameimarika na kukua zaidi.”
Pia Mhe. Chana amefafanua kuwa biashara baina ya nchi hizi mbili imekuwa
ikiimarika kila siku kwani Afrika Kusini wamekuwa wananuzi wakubwa na
maparachichi yanayotoka hapa nchini kwetu lakini pia Tanzania imekuwa ikinunua
juisi nyingi kutoka Afrika Kusini pamoja na bidhaa nyingine.
Akiongelea umuhimu wa kutumia lugha ya Kiswahili Mhe. Chana amesema “ni
wakati mzuri sasa kueneza lugha ya Kiswahili iwe lugha yetu kuu ya mawasiliano
kwa nchi zote za Kusini mwa Afrika na pia bara zima la Afrika.
Mhe. Chana ameishukuru Kamati hiyo kwa kuja Tanzania kujifunza mambo
mengi, na amewaasa wapate nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo
hapa nchini hasa mbuga za wanyama na vivutio vingine.
Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. William Shabalala amesema “Uhusiano
baina ya Tanzania na Afrika Kusini hauwezi kusahaulika, na hauwezi kusema
chochote kuhusu Uhuru wa Afrika Kusini pasipo kutaja Tanzania maana sisi tuna
ndugu Morogoro ambao walipigania Uhuru wakitokea hapa nyumbani Tanzania. Na
malengo yetu ya kuja hapa pia ni kujifunza mambo mbalimbali mnayoyafanya maana
kwetu Tanzania ni nchi muhimu sana.”
Pia, aliongeza “tunajivunia sana kuwa tupo nyumbani na katika maisha ya
sasa ni vyema kizazi chetu kijue kuwa wapi tumetokea na wapi tunaelekea hasa
katika mahusino ya nchi hizi mbili, Walichokifanya Waasisi wa Uhuru wetu
Mandela na Nyerere ni kitu cha thamani sana ambacho kimetufanya tuwe pamoja
mpaka sasa.”
Comments
Post a Comment