NAIBU WAZIRI GEKUL APOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA CHUO CHA IJA

 


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akipitia ripoti ya Utekelezaji wa shughuli za Chuo cha Mahakama Lushoto wakati ikiwasilishwa na Naibu Mkuu wa chuo Dkt. Goodluck Chuwa, tarehe 18 Oktoba, 2023 Jijini Dodoma.

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Na George Mwakyembe – WKS Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amepokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za chuo cha Mahakama Lushoto na kuwaasa kufungua matawi ya chuo maeneo mengine nchini kama vile Dodoma na baadhi ya maeneo mengine.

Mhe. Gekul amepokea taarifa hiyo tarehe 18 Oktoba, 2023 Jijini Dodoma na kuwaasa kuwa ni vyema sasa chuo cha Mahakama Lushoto kikawa na matawi katika mikoa mbalimbali ili kuruhusu watoto wengi wa kitanzania kusoma chuo hicho. Aidha, Gekul amefafanua kuwa mbali ya kutoa mafunzo ya Majaji lakini pia chuo hicho kijikite katika kutoa mafunzo katika kada nyingine za sheria kama vile mafunzo kwa Makatibu wa Majaji na pia mafunzo kwa wanasheria.

Naye Naibu Mkuu wa chuo kwa upande wa Taaluma, Tafiti na Ushauri elekezi Dkt. Goodluck Chuwa ameeleza kuwa tayari wamejipanga kuandaa programu mbalimbali ambazo zimekuwa zikihitajika katika jamii, na kuahidi kuwa chuo kimelibeba wazo la kufungua matawi sehemu zingine za nchi.

Katika historia ya nchi, Chuo cha Mahakama Lushoto ndicho chuo pekee kinachotoa mafunzo kwa Majaji pamoja na Mahakimu.


Comments

Popular posts from this blog

USAJILI WA VIZAZI NA VIFO NI TAKWA LA KISHERIA

UONGOZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINADAMU NA WATU YAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

BODI YA KITAIFA YA USHAURI YA MSAADA WA KISHERIA YATEMBELEA WASAIDIZI WA KISHERIA IRINGA