Serikali Itaendelea Kuimarisha Michezo – Dkt Biteko
Naibu
Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko akikagua wachezaji wa timu za mpira wa miguu
kati ya timu wa Mahakama na Timu ya Wizara ya Kilimo kwenye mashindano ya SHIMIWI mkoani Iringa tarehe
04 Oktoba 2023.
Watumishi
wa Wizara ya Katiba na Sheria wakiwa katika maandamano ya ufunguzi wa
mashindano ya michezo ya SHIMIWI Mkoani Iringa tarehe 04 Oktoba, 2023.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na George Mwakyembe – WKS Iringa
Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Dotto Biteko amesema
Serikali itaendelea kuimarisha michezo kwa watumishi wote nchini ili kujenga
mahusiano mazuri baina yao lakini pia kuimarisha afya.
Mhe. Biteko ameyasema hayo alipokuwa akizindua michezo
ya SHIMIWI inayofanyika Mkoani Iringa tarehe 04 Oktoba 2023. Michezo hii ambayo
inajumuisha watumishi wa Wizara, Idara pamoja na Taasisi mbambali za umma imeanza
tangu tarehe 29 Septemba, 2023 kwa michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono
pamoja na kuvuta kamba.
Mhe. Biteko amesema “Michezo hii ya SHIMIWI ni ya
watumishi wa Serikali, tusiruhusu iharibiwe kwa kuingiza mamluki ambao siyo
watumishi. Serikali imeleta hii michezo ili watumishi muweze kuimarisha afya
lakini pia kuleta hari mpya mahala pa kazi,”
Aidha, Dkt. Bitteko amewaasa Makatibu wote wa Wizara
pamoja na Wakurugenzi wa Taasisi pamoja na Idara kusimamia kikamilifu michezo
mahala pa kazi na kuwaruhusu watumishi kushiriki kwenye michezo mbalimbali kwa
kuwajengea mazingira mazuri ya ushindani.
Naye Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Daniel Mwalusamba amefafanua kuwa michezo hii ni ya 37 na imejumuisha jumla ya watumishi 2,765 ambao wanatoka kwenye Wizara 24, Taasisi za Serikali 14 pamoja na Wakala wa Serikali 5 wote wamejisajili katika michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta kama na kukimbia.
Bw. Mwalusamba amewashukuru Makatibu Wakuu wote pamoja na Wakuu wa Taasisi za Umma kwa kuwaruhusu watumishi kushiriki michezo ya SHIMIWI na kuamini kuwa mwaka ujao watawaruhusu watumishi wengi zaidi.
Comments
Post a Comment