Tukitekeleza Kazi kwa Kasi Hii Tutaelewana: Dkt. Chana
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.
Pindi Chana, Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul wakati wakipokea taarifa ya
utekelezaji wa Robo Mwaka na Muswada wa marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya
sheria, tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma.
Sehemu ya Viongozi wa taasisi walishiriki kikao kazi cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Robo Mwaka na Muswada wa marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya sheria, tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi tarehe 17 Oktoba, 2023 Ofisi za Wizara Dodoma.
Na
William Mabusi – WKS Dodoma
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt.
Pindi Chana amepokea taarifa za utekelezaji za Robo Mwaka ya Mwisho kwa mwaka
wa fedha 2022/23 na Robo Mwaka ya Kwanza kwa mwaka 2023/24 kutoka taasisi zilizo
chini ya Wizara na kuzipongeza kwa kazi nzuri na utekelezaji wa majukumu ya
taasisi hizo kwa wakati.
Mhe. Chana ametoa pongezi hizo wakati yeye na
Naibu Waziri Mhe. Pauline Gekul walipokutana na Watendaji kutoka Taasisi hizo
na Menejimenti ya Wizara tarehe 17 Oktoba, 2023 kwenye ofisi za Wizara Mtumba
Dodoma.
“Kazi mlizofanya
zinatoa alert, ni taarifa
chunguzi za ukweli na zinazoonesha haki imekuwa ikitendeka,” alisema
Mhe. Waziri na kwa namana ya pekee amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya sheria
na kuahidi kwamba Wizara yake itaendelea kusimamia utoaji haki na kutekeleza
maono ya Mhe. Rais ya kutaka haki sawa kutolewa na kwa wakati.
Katika kikao kazi hicho pia Mhe. Waziri alipokea Muswada wa
marekebisho mbalimbali kwenye sekta ya sheria yenye Sehemu Ishirini na nne yanayolenga
kuweka mazingira wezeshi katika kuendelea kutekeleza majukumu kwa wakati, kuzuia
matumizi mabaya ya mali ya uma, kuondoa changamoto ya tafsiri kwa baadhi ya
sheria na hivyo kuondoa mkanganyiko katika kutekeleza sheria hizo ili kuboresha
utoaji wa haki na hivyo kuongeza ufanisi wa kazi.
Katika hatua nyingine Mhe. Waziri alikutana na
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi na kujadili
masuala mbalimbali ya kuboresha ya sekta ya sheria na utoaji haki.
Akichangia katika kikao kazi hicho Naibu Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe. Gekul aliitaka Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora itumie sehemu ya utawala bora kuandaa mafunzo kwa viongozi wa ngazi
za chini za utawala wakati nchi inajiandaa na Uchaguzi
wa Serikali za Mtaa mwakani. Aidha, Mhe. Gekul ameitaka Tume hiyo kuwa na mkakati wa kuwafikia wananchi wa
chini kabisa. “Kiu yangu ni
kuona mna Maafisa kwenye kila mkoa ili kuwarahisishia wanachi kuwafikishia kero
zao,” alisema.
Comments
Post a Comment