SALVA KIIR MAYARDIT AWASILI NCHINI NA KULAKIWA NA DKT. CHANA

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakikagua gwaride la heshima, tarehe 23 Novemba, 2023 mara baada ya kuwasili nchini. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana na Mgeni wake Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit mara baada ya kuwasili nchini, tarehe 23 Novemba, 2023 Jijini Arusha. XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir Mayardit amewasili nchini tarehe 23/11/2023 na kupokewa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana kushiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Jijini Arusha. Mara ya mwisho Rais Salva Kiir kuja nchini ilikuwa April 15, 2016 ambapo alikutana na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya utiaji saini wa Mkataba wa Sudani Kusini kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huo unahudhuriwa ...