KASI YA UJENZI IENDANE NA UBORA: DKT. CHANA

Mhandisi Nassiri Nassoro akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la Wizara kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Pindi Chana, tarehe 17 Novemba, 2023


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara, tarehe 17 Novemba, 2023

 XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na William Mabusi – WKS Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara ambao umefikia asilimia 79 linaojengwa Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, na kumtaka Mkandarasi kuongeza kasi huku akizingatia ubora.

Ukaguzi huo ameufanya tarehe 17 Novemba, 2023. “Kwenye ujenzi wa majengo haya tunashindana hivyo ukiona mwenzio ameweka vioo nawe unajiuliza la kwangu linawekwa vioo lini,” alisema Dkt. Chana huku akitahadharisha pamoja na mambo mengine upatikanaji wa maji kwenye jengo akitaka kuwepo na uwiano wa idadi ya watumishi na uwezo wa pampu ya kusukumuia maji ili yafike kwenye sakafu zote za jingo

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA