MAHAKAMA YA MWANZO YA TARAFA YA BWAKILA CHINI KUJENGWA – MHE GEKUL


Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akijibu swali Bungeni leo tarehe 07 Novemba 2023, Bungeni Jijini Dodoma. 

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na, George Mwakyembe- WKS – Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amefafanua kuwa Serikali katika mwaka fedha 2023/ 2034 imejipanga kujenga Mahakama zaidi ya 60 nchini na katika idadi hiyo pia ipo mahakama ya mwanzo ya tarafa ya Bwakila chini.

Mhe Gekul ameyasema hayo leo tarehe 07/11/2023 bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Morogoro Kusini Mhe Innocent Edward Kalongoles alitetaka kujua ujenzi wa mahakama katika eneo hilo utafanyika lini. Mhe Gekul amefafanua kuwa tayari zabuni imetangazwa kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mahakama hiyo na wakati wowote atatangazwa na kuanza kazi.

Aidha, Mhe Gekul ameleza kuwa Mahakama ya mwanzo ya Matombo na Namvua zina majengo ya ambayo ni chakavu na tayari Serikali imeyaweka katika mpango wa ukarabati katika mwaka wa fedha 2024/2025 mpango ambao utajumisha na ukarabati wa Mahakama zingine nchini.

Pia Mhe. Gekul ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mhe   Dkt. Samia Suluhu Hassan imetoa ziadi ya billion 88 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa Mahakama ili haki ipatikane kwa wakati. Hivyo amemtoa wasiwasi mbunge huyo wa Mororgoro kusini na kuhaidi kuwa Mahakama itajengwa kwa wakati. 

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA