TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria leo tarehe 6 Novemba 2023 Jijini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana akitoa ufafanuzi wa Jambo alipkuwa akiongea na   watumishi wa Wizara ya katiba na sheria leo 6 Novemba 2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul akiongea na watumishi wa Wizara ya Katiba na Sheria   leo tarehe 6 Novemba 2023 Jijini Dodoma.

Watumishi wa Wizara ya Katiba wakimsikiliza waziri alipokuwa akiongea kwenye kikao kazi kilichofanyika leo tarehe 6 Novemba 2023 mtumba jijini Dodoma

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Na. George Mwakyembe – WKS – Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt Pindi Chana amewataka watumishi pamoja na menejimenti ya Wizara yake kufanya kazi kwa kujituma, uadilifu na kwa ushirikiano ili kutimiza malengo ya Wizara katika kuwahudumia watanzania.

Waziri Chana ameyasema hayo leo tarehe 06/11/2023 Mtumba Jijini Dodoma yalipo Makao Makuu ya Wizara hiyo alipokutana na wafanyakazi na Menejimenti ya Wizara na kufanya nao kikao kazi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara. Akiongea kwenye kikao hicho Mhe Chana alisema “dhamana tuliyopewa ya kuwahudumia wananchi ni kubwa na lazima tufanye kazi kwa bidii lakini pia kwa kujituma huku tukizingatia uadilifu na uaminifu”

Aidha, Mhe Balozi Chana ameongeza kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ni moja kati Wizara kongwe na muhimu sana hasa katika kusimamia sheria za nchi, na tayari tunaendelea na mchakato wa kutafsiri sheria zote za nchi na kuhakikisha sheria zote zinandikwa kwa lugha ya Kiswahili.

Naye Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul amewataka watumishi kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa kujituma. Akiongea kwenye kikao hicho Mhe. Gekul amefafanua kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ina kazi nyingi za kuwahudumia wananchi ambazo zote ni za kutatua matatizo yao hivyo lazima tuwe wabunifu na wavumilivu na wenye lugha nzuri.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Bi Mary Makondo amefafanua kuwa mbali ya kuwa ikama ya watumishi ni 205 lakini tayari Wizara imendelea kupokea watumishi ambao wamekuwa wakihamia kutoka sehemu mbalimbali na kuongeza nguvu katika utendaji. Bi, Makondo ameongeza kuwa sisi kama watumishi tumeakuwa tukiishi kama familia na kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ikiwemo kuwa na mfuko wa kusaidiana pale mtumishi anapopata tatizo. 

Pia Bi Makondo amemshukuru Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa kushirki kwenye kikao cha pamoja na watumishi na kuhaidi ushirikiano na mshikamano katika utendaji kazi.  

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN