WAZIRI CHANA AIPONGEZA NMB KWA KUTOA HUDUMA ZINAZOIGUSA JAMII

 





Waziri wa Katiba na  Sheria  Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na  Wanasheria Binafsi katika mkutano uliofanyika leo tarehe 10 Novemba Jijini Dar es Salaam .

Waziri wa Katiba na  Sheria  Mhe Balozi Dkt Pindi Chanaajiongea na   Wanasheria Binafsi kwenye  mkutano uliofanyika leo tarehe 10 Novemba Jijini Dar es Salaam .



Waziri wa Katiba na Sheria  Mhe. Balozi   Dkt Pindi Chana  akipokelewa na mwenyeji wake Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB kwenye mkutano wa NMB na Taasisi za Sheria Mkoa wa Dar es salaam. 


Waziri wa Katiba naSheria  akiongoza na Mhe Omary Said Shabani  Waziri wa Viwanda na Biashara Zanzibar  baada ya Kuwali kwenye Mkutano wa NMB  na Taasisi  za Sheria  Mkoa wa Dar es Salaam. 

Na Lusajo Mwakabuku – WKS

Waziri wa Katiba n Sheria Mhe.Balozi Dkt Pindi Chana Ameshiriki Mkutano wa NMB na Taasisi za Sheria za Mkoa wa Dar es Salaam na Kuipongeza Benki hiyo kwa kuendelea kufanya kazi kwa Weledi na kuiomba kuendelea kushiriki kwenye Huduma mbali mbali zinazogusa jamii.

Akisoma hotuba yake, Waziri Chana ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo aliwaomba NMB na Wanasheria kuunga mkono Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign) kwa hali na mali kwa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji kurudisha kwa jamii (Corporate Social Responsibility).

Waziri Chana aliongeza kuwa kampeni hii inakusudia kutoa elimu ya sheria nchi nzima pamoja na msaada wa kisheria itakayojenga taifa la watu wenye ufahamu wa sheria hivyo watu wataacha kukopa mikopo ya kausha damu au vikoba vya kuficha fedha uvunguni na kuja kukopa benki ambapo napo watahitaji huduma ya wakili kuthibisha mikopo yao.

Mkutano huo ulioudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mh Omary Said Shaabani ambae amesema NMB imekua chachu kwa maendeleo ya ya Viwanda na Biashara kwa ujumla na kuitaka iongeze huduma kwa upande wa Zanzibar.

Aidha  Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Ruth Zaipuna ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki yanayowezesha huduma za Benki kukua kwa kiasi kikubwa.




Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA