WAZIRI CHANA ASHIRIKI KIKAO CHA BARAZA LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


 Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akishiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 22 Novemba, 2023 Jijini Arusha.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana akishiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki, tarehe 22 Novemba, 2023 Jijini Arusha.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana anashiriki Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyikia Jijini Arusha.

Mkutano huo ulioanzia katika Ngazi ya Wataalam waliokutana Jijini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2023 na ukafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 21 Novemba 2023, kinakamilishwa na Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri ulioanza leo tarehe 22 Novemba 2023.

Masuala yanayojadiliwa katika Mkutano huo wa wataalam ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 hadi 24 Novemba, 2023; Taarifa ya utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya kuhusu; Majadiliano ya Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya; Hatua iliyofikiwa katika kutafuta amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo ya mchakato wa kijeshi na uongezaji muda wa mkataba wa SOFA; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya ya Afrika; majadiliano ya Katiba kuhusu Katiba ya Fungamano la Kisiasa Afrika Mashariki; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na; Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya Uandishi wa insha kwa wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YAIPONGEZA WIZARA KWA UTEKELEZAJI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN

TUFANYE KAZI KWA UADILIFU NA USHIRIKIANO - MHE CHANA